Ishara Za Mapema Za Mimba Na Wakati Zinapo Anza Kuonekana

Ishara Za Mapema Za Mimba Na Wakati Zinapo Anza Kuonekana

Matiti hubadilika na kuhisi laini zaidi, kufura ama kuuma kufuatia ongezeko la homoni mwilini. Mabadiliko haya huanza kufanyika kutoka wiki ya 4 hadi ya 6.

Kipimo cha mimba na kufanya ultrasound ndizo njia hasa za kufahamu iwapo mwanamke ana mimba ama la. Kujua ishara za mapema za mimba zinaweza saidia kujua mwanamke anapokuwa mjamzito. Mbali na kukosa kipindi cha hedhi, kuna ishara zingine ambazo zina ashiria kuwepo kwa mimba. Unafahamu dalili za mimba huanza kuonekana lini?

Ishara za mimba huanza kuonekana lini?

Umri wa mimba hulingana na wakati mama alianza kupata kipindi cha hedhi. Hiyo ndiyo inayo fahamika kama wiki ya kwanza ya ujauzito, hata kama bado hauna mimba. Wakati unapo tarajia kujifungua huhesabiwa wiki 40 baada ya siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho.

Dalili za mimba na wakati zinapo anza kushuhudiwa

dalili za mimba huanza kuonekana lini

  • Kukosa hedhi

Yai linapo jipandikiza kwenye kuta za uterasi, homoni hutolewa mwilini na kudhibiti ovari kuto toa yai lingine. Na kumfanya mwanamke kukosa kupata hedhi ya kila mwezi. Mimba inapotungwa, mwili hutoa kichocheo cha hCG kinacho uegemeza ujauzito.

Unapokosa kipindi chako cha hedhi, ni vizuri kufanya kipimo cha nyumbani cha mimba. Vipimo hivi hugundua kuwepo kwa homoni ya mimba ya hCG. Kinapo dhibitisha kipimo chanya, wasiliana na daktari ili uanze kliniki.

  • Kuumwa na tumbo na matone ya damu

Dalili hizi huonekana kati ya wiki ya kwanza hadi ya nne ya ujauzito. Mabadiliko katika kipindi hiki huwa yana tendeka kwenye seli. Matone ya damu yanayo toka baada ya yai kujipandikiza kwenye kuta za uterasi ni tofauti na damu ya hedhi.

Damu hii huwa ya rangi ya pinki ama hudhurungi. Huwa nyepesi na huisha kwa kupunguza kutumia tishu. Uchungu sio mwingi sana ikilinganishwa na uchungu wa hedhi. Na kwa wastani hutoka kwa siku tatu.

  • Mpigo wa moyo ulioongezeka

Katika wiki ya 8 hadi ya 10, moyo wa mwanamke huanza kupiga kwa kasi zaidi. Husababishwa na ongezeko la homoni mwilini.

  • Kichefuchefu na ugonjwa wa asubuhi

chumvi kupima mimba

Katika wiki ya 4 ama ya 6 ya ujauzito, mwanamke huanza kuhisi kichefuchefu na ugonjwa wa asubuhi na pia kutapika. Ishara hizi hushuhudiwa wakati wowote ule wa mchana. Mwanamke ana shauriwa kunywa maji mengi ili kupunguza dalili hizi.

  • Mabadiliko ya matiti

Mabadiliko haya hufanyika kati ya wiki ya 4 hadi ya 6. Matiti hubadilika na kuhisi laini zaidi, kufura ama kuuma kufuatia ongezeko la homoni mwilini. Wiki chache baada ya mwili kuzoea viwango vipya vya homoni, ishara hizi hufifia.

Katika wiki ya 11, rangi ya chuchu hukolea zaidi na kuwa kubwa zaidi.

Ikiwa ulikuwa na shaka dalili za mimba huanza kuonekana lini, makala haya yamekuelimisha zaidi kuhusu dalili unazo paswa kuangazia na wakati upi.

Soma Pia:Je, Masi Rutuba Inaweza Saidia Na Kutunga Mimba?

Written by

Risper Nyakio