Dalili za mimba kwa wanaume kama kuhisi kichefuchefu, kuwa na mhemko wa hisia, kuongeza uzito ama kujaa gesi tumboni hufahamika kama couvade. Hali ya mimba ya huzuni. Hali hii imekuwepo kwa muda mrefu, hata kama sio watu wengi wanaofahamu kuihusu. Utafiti wa kina haujafanyika katika nyanja hii, ila, katika miaka michache iliyopita, watafiti wameanza kufanya utafiti kuihusu.
Dalili Za Mimba Kwa Wanaume

Ni vigumu kufahamu visa vya utendekaji wa couvade kwani wanaume wengi hawaripoti wanapopata dalili hizi. Kulingana na ripoti iliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Newfoundland, wake walioulizwa kuhusu dalili hizi katika waume zao, asilimia zaidi iliripotiwa. Tofauti na wanaume walipoulizwa kuhusu dalili hizo. Kuna uwezekano kuwa wanaume hawako makini na dalili hizi kwani hawaamini kuwa wanaweza kupata dalili za mimba.
Wajawazito kwenye jamii wanahimizwa kuzungumza kuhusu safari yao ya mimba, dalili wanazopata na kadhalika. Mwanamke anapokuwa na mhemko wa hisia katika mimba ama kutamani vyakula tofauti, bwanake atakuwa na huruma kwake. Hisia hizi za huruma nyingi zitaibua dalili za couvade kwa wanaume na kumfanya bwana kuwa na utangamano wa karibu na mtoto wake.

Mabadiliko ya viwango vya homoni. Utafiti umedhihirisha kuwepo kwa tofauti katika viwango vya homoni miilini ya wanaume wanaotarajia, waliokatika uhusiano na walio peke yao. Homoni ya testosterone huwa chini kwa wanaume walio katika uhusiano. Haijulikani iwapo viwango hivi hupungua punde tu baada ya uhusiano kuanza na muda baadaye katika uhusiano. Homoni ya prolactin huwa juu zaidi katika wanaume wiki chache baada ya kuzaliwa kwa mtoto.
Dalili za mimba kwa wanaume ama couvade zinazidi kufanyiwa utafiti kubaini vyanzo na iwapo wanaume wote hupata ishara hizi hata bila ufahamu wao. Ni dhabiti kuwa mimba huathiri wanandoa wote wawili. Hata bila ufahamu wa wanaume, wanapata hisia za huzuni na utangamano na wake zao kuzidi wanapokuwa na mimba.
Chanzo: Parenting
Soma Pia: Ishara 5 Zinazo Dhibitisha Kuwa Mwanamme Ni Baba Mwema Kwa Watoto Wake