Mambo 5 Unayo Paswa Kujua Kuhusu Mimba Ya Mapacha

Mambo 5 Unayo Paswa Kujua Kuhusu Mimba Ya Mapacha

Mimba ya mapacha ina hitaji kuangaliwa zaidi ikilinganishwa na mimba ya mtoto mmoja. Mapacha wana stahili ultrasounds na vipimo zaidi.

Je, unafahamu dalili zipi za mimba ya mapacha? Ni sawa na mimba ya mtoto mmoja ama kuna tofauti? Soma zaidi upate maarifa kuhusu jinsi mimba ya mapacha ilivyo tofauti na ya mtoto mmoja.

Dalili za mimba ya mapacha

dalili za mimba ya mapacha

1.Ugonjwa wa asubuhi ulio zidi

Tofauti na mimba ya mtoto mmoja, mimba ya mapacha ina ugonjwa wa asubuhi zaidi kwani mama ana viwango vingi zaidi vya homoni ya human chorionic gonadotropin (HCG). Na kumfanya mama ashuhudie kichefu chefu na kutapika zaidi katika trimesta yake ya kwanza. Habari njema ni kuwa, ishara hizi zitaanza kupunguka mama anapo fika wiki ya kumi na nne.

Mama pia ata hisi kuumwa na mgongo zaidi kwa sababu ana beba uzito wa watoto wawili. Kulala kutamtatiza pamoja na kuhisi kiungulia.

2. Kutoa damu zaidi

Unapo vuja damu sana katika trimesta ya kwanza, hiyo ni ishara ya kukutia wasi wasi kwani huenda ukawa unapoteza mtoto. Kuharibika kwa mimba kuna shuhudiwa sana kwa mama aliye na mtoto zaidi ya mmoja.

Lakini, kutoa kiasi kidogo cha damu sio sababu kubwa ya kuwa na wasiwasi hata kama una tarajia mimba ya watoto zaidi ya mmoja. Kiwango cha damu kwa mama mwenye mimba ya mapacha kitakuwa kingi ikilinganishwa na mama mwenye mimba ya mtoto mmoja.

3. Ongezeko la uzito mwingi

Na watoto mapacha, wamama huongeza uzito zaidi kwani unahitaji placenta mbili na kiwango kikubwa cha uowevu wa amniotic utakao walinda watoto wawili. Hauli chakula chako na cha mtoto mmoja, mbali ni chakula kitakacho kutosha pamoja na watoto wawili. Kwa hivyo bila shaka utashuhudia ongezeko zaidi la uzito. Hata hivyo haupaswi kuongeza uzito zaidi ya kilo 27 ukiwa na mimba ya mapacha. Wasiliana na daktari wako akushauri uzito unao paswa kuongeza kulingana na uzani wako.

Mambo ya kufahamu kuhusu mimba ya mapacha

dalili za mimba ya mapacha

You can conceive twins naturally with these criteria.

1. Kuhisi mateke ya mapacha tumboni

Sawa na mimba ya mtoto mmoja, unaanza kuhisi mateke ya mtoto ama mwendo wa mtoto tumboni unapo fikisha kati ya wiki ya 18 hadi ya 20. Hakuna kinacho badilika katika mwendo wa watoto tumboni hata wanapokuwa mapacha.

2. Utamtembelea daktari wako mara zaidi

Mimba ya mapacha ina hitaji kuangaliwa zaidi ikilinganishwa na mimba ya mtoto mmoja. Mapacha wana stahili ultrasounds na vipimo zaidi.

3. Utahitaji folic acid zaidi

Folic acid ni muhimu sana katika mimba ili kuhakikisha kuwa mtoto hapati changamoto zozote za kuzaliwa. Mama atahitaji kuchukua kiwango zaidi cha folic acid ili kuwaokoa watoto wote wawili, kiwango kinacho shauriwa kwa mapacha ni miligramu moja kila siku.

4. Nafasi zaidi za upasuaji wa C-section

Kwa watoto mapacha, kuna nafasi zaidi ya mama kujifungua kwa njia ya upasuaji wa C-section. Kuna uwezekano zaidi wa mtoto kuwa katika njia isiyo faa kabla ya kujifungua, miguu huenda ikawa iko chini, na njia asili ni pale ambapo kichwa cha mtoto kinafaa kuwa chini ili kitoke kwanza.

5. Uchungu wa uzazi kuanza mapema

Wamama wengi walio na mimba ya mapacha hushuhudia uchungu wa uzazi wanapokuwa wiki 36-37 ya ujauzito. Wakati ambapo kwa mimba ya mtoto mmoja, huanza katika wiki ya 40. Kuzaliwa mapema kwa mapacha kuna waweka katika hatari ya kupata matatizo ya kupumua. Pia, huenda wakazaliwa na uzani wa chini na kuugua matatizo mengine ya kiafya.

Soma PiaUnapata mapacha, kulingana na ishara hizi za hadithi za kuambiwa

Written by

Risper Nyakio