Kwa kawaida mama anaposhika mimba jinsia ya mtoto huwa swali la kwanza kabisa. Hii ni kwa kuwa husaidia katika kujipanga. Kwa mara nyingi ultrasound huonyesha jinsia ya mtoto afikiapo umri wa wiki ishirini. Ila kuna njia asili za kudadisi mimba ya kike. Soma zaidi kufahamu dalili za mimba ya mtoto msichana.
Dalili Za Mimba Ya Mtoto Msichana

- Kubadilika badilika kwa mihemko ya hisia
Jinsia ya mtoto ambaye hajazaliwa husababisha mabadiliko ya tabia kwa mama. Kina mama wenye hasira huashiria mtoto wa kike.
Iwapo mwanamke ataongeza uzani kwa ghafla anatarajia mtoto wa kike. Ila hakuna utafiti kuhakiki hili.
Hukisiwa kuwa iwapo mama anapenda sukari ni dalili ya kubeba mtoto wa kike na wale wanaopendelea chumvi ni dalili ya kubeba mtoto wa kiume.
Mama aliyebeba mimba huwa na utofauti kwa ngozi yake kutokana na ongezeko la homoni. Nywele nyembamba na zinazokatika huwa ishara ya mtoto wa kike. Nywele zinazongaa na kuvutia ni ishara za mtoto wa kiume.
Kwa wengi huweza kupata homa ya asubuhi ama morning sickness. Ila wengi hudhani kuwa makali kwenye homa hii au kichefuchefu huashiria mtoto wa kike.
- Mipigo ya moyo ya haraka ya mtoto
Wengi huweza kuamini kuwa mipigo ya moyo ya haraka ya mtoto huashiria kuwepo kwa mtoto wa kike.

Chuchu ni sehemu mojawapo ya mama ambayo huwez kubadilika wakati wa ujauzito. Husemwa kuwa iwapo chuchu zitabaki ile rangi yake uwezekano ni mtoto wa kike na iwapo zitakoloe na kuwa kiza zaidi ni ishara ya mtoto wa kiume.
Mkao wa tumbo ni ishara moja ya kugundua jinsia ya mtoto. Husema kuwa iwapo tumbo la ujauzito litakuwa juu ama katikati ni ishara ya mtoto wa kike na ikiwa litakuwa chini ni dalili ya mtoto wa kiume.
Kwa mama anayetarajia mtoto wa kike titi la kushoto huwa kubwa kuliko lile la kulia. Pia ongezeko la ghafla kwa matiti huwa dalili ya mtoto wa kike.
Kutokwa na chunusi usoni huwa dalili mojawapo ya ishara ya kujifungua mtoto wa kike.
Wakati wa ujauzito huwa na machovu sana. Na iwapo wakati wa kupumzika unalalia ubavu wa kulia ni ishara ya mtoto wa kike.
Kwa muda watu wameweza kuchunguza kwa uhakika dalili za mimba ya mtoto msichana. Hizi husaidia kujipanga ata kabla ya matokeo ya ultrasound.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Kuna Tofauti Kati Ya Tabia Ya Mtoto Wa Kiume Tomboni Na Ile Ya Wa Kike?