Dalili Za Mimba Ya Kiume: Jinsi Ya Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Unaye Mtarajia

Dalili Za Mimba Ya Kiume: Jinsi Ya Kufahamu Jinsia Ya Mtoto Unaye Mtarajia

Kufahamu jinsia ya mtoto ni jambo la kusisimua. Ili kuwa na uhakika, unashauriwa kungoja hadi baada ya wiki 9 ili kubaini kwa kweli!

Punde tu mimba yako inapo anza kuonekana, utapata ushauri mwingi kuhusu mimba na unavyo paswa kuitunza. Kitu kingine ambacho huenda ukasikia ni kuhusu jinsia ya mtoto unaye tarajia. Hii ni mada kuu na utasikia mambo tofauti kuhusu ishara unazo paswa kuangalia kwa makini ili ujue ikiwa unatarajia mtoto wa kiume ama wa kike. Tazama imani kuhusu dalili za mimba ya mtoto wa kiume na jinsi halisi ya kufahamu jinsia ya mwanao.

Imani kuhusu dalili za mimba ya mtoto wa kiume

dalili za mimba ya mtoto wa kiume

Ugonjwa wa asubuhi

Kuna imani kuwa wingi wa ugonjwa wako wa asubuhi ni ishara ya jinsia ya mtoto unaye tarajia. Kwa mama anaye tarajia mtoto wa kiume, hatasumbuliwa sana na ugonjwa wa asubuhi. Kwa wanawake wanao tarajia watoto wa kike, ugonjwa wa asubuhi utakuwa mwingi. Hii ni kwa sababu kuna aminika kuwa, mimba ya kike huwa na homoni zaidi.

Ugonjwa wa asubuhi huwa tofauti kwa kila mama na pia hutofautiana kwa kila ujauzito.

Hamu ya vyakula

Unapo tarajia mtoto wa kike, una tamani vitu vitamu kama switi na chokleti. Huku ukitarajia msichana, ulimi wako utatamani vitu vilivyo na chumvi kama vile pickles ama vyakula chachu.

Umbo la tumbo

Watu wana amini kuwa, tumbo yako inapokuwa chini, nafasi kubwa ni kuwa huyo ni mtoto wa kiume. Ukweli ni kuwa, huku kuna lingana na uterasi ya mama na kila tumbo na uterasi huwa na umbo lake hasa.

Hali ya ngozi ya mama katika ujauzito

upele baada ya kujifungua

Unapokuwa mjamzito kisha upate upele usoni, kuna imani kuwa una tarajia mtoto wa kike na yeye ndiye aliye iba urembo wako. Huku unapo tarajia mtoto wa kiume, huenda ngozi yako ikabaki sawa ama ikawa laini zaidi.

Kuna baadhi ya wanawake wanao shuhudia kung'aa katika mimba. Huenda nywele yao pia ika ng'aa, hii ni ishara kuwa unatarajia mtoto wa kiume huku nywele yako inapo kuwa imeshikana sana unatarajia msichana. Kumbuka kuwa hii ni imani tu na hakuna utafiti wa kuegemeza maneno haya.

Mbinu hasa za kufahamu jinsia ya mtoto

Njia tatu hasa zinazo fahamika kumsaidia mzazi kujua jinsia ya mtoto ni:

  1. Kipimo cha damu cha seli za dna 

Kipimo hiki kinaweza fanyika mama anapo fikisha wiki 9 za ujauzito. Ikiwa mtoto aliye tumboni ana matatizo yoyote, pia kipimo hiki kitasaidia kugundua.

2. Ultrasound

Kipimo hiki kina fanyika katika wiki ya 18 na ya 20. Na kina saidia kujua jinsia ya mtoto na ikiwa ako mahali panapo faa.

Kufahamu jinsia ya mtoto ni jambo la kusisimua. Ili kuwa na uhakika, unashauriwa kungoja hadi baada ya wiki 9 ili kubaini kwa kweli!

Soma Pia:Mambo Ya Kufanya Ili Upate Mtoto Wa Kike Mrembo

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio