Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ukuaji Wa Fetusi Na Dalili Za Mimba Ya Mwezi Mmoja

2 min read
Ukuaji Wa Fetusi Na Dalili Za Mimba Ya Mwezi MmojaUkuaji Wa Fetusi Na Dalili Za Mimba Ya Mwezi Mmoja

Dalili za mimba ya mwezi mmoja huwa nyepesi. Huenda mwanamke akakosa kufahamu ana mimba katika mwezi huu. Hasa kama ni mimba isiyopangwa.

Dalili za mimba ya mwezi mmoja huwa nyepesi. Huenda mwanamke akakosa kufahamu ana mimba katika mwezi huu. Hasa kama ni mimba isiyopangwa, mwanamke huenda akachukulia dalili hizi kuwa za kukaribia kwa siku ya kupevuka kwa yai.

Dalili za mimba ya mwezi mmoja

Dalili za mimba ya mwezi mmoja

Kukosa hedhi. Kukosa hedhi ni dalili ya mimba iliyo maarufu zaidi. Wanawake walio na vipindi vya hedhi vilivyo vya kawaida wanaweza kufahamu kwa urahisi mabadiliko mepesi yanayofanyika mwilini. Hata hivyo, kuna sababu zingine kama kubadilisha lishe, kufanya mazoezi ama kusafari ambazo zinaweza kufanya kipindi cha hedhi kichelewe.

Kuvimbiwa tumbo. Ongezeko la homoni mwilini humfanya mwanamke ahisi kuvimbiwa. Baada ya kipindi cha hedhi, mwanamke huwa na ishara sawa. Huenda akachanganya ishara hii ya mimba na dalili za PMS. Ili kutatua hali hii, anapaswa kufanya mazoezi na kula chakula chenye faiba.

Maumivu ya tumbo. Kuna baadhi ya wanawake wanaopata maumivu ya tumbo yasiyodumu kwa muda mrefu wanapotunga mimba. Kwa sababu mama bado hajafahamu kinachoendelea, nafasi kubwa ni kuwa atapuuza ishara hii na kuchukua dawa za kupunguza maumivu ya tumbo.

Mhemko wa hisia. Homoni zinapozidi mwilini, mwanamke huathiriwa kihisia ama kifizikia. Homoni za ujauzito humfanya mwanamke awe na hisia tele zinazobadilika mara kwa mara. Hisia kama kuwa na furaha, kuhisi kulia, kuwa na wasiwasi tele. Ni vyema kwa mwanamke kuzungumza na marafiki zake ama mtaalum kuhusu hisia zake.

dalili za mimba ya mwezi mmoja

Kuvuja damu. Kuvuja damu hufanyika yai lililorutubishwa linapopandikiza kwenye mji wa mimba. Siku kati ya 6 na 12 baada ya tendo la ndoa, mama huvuja damu ya implantation. Sio wanawake wote wanaovuja damu ya implantation. Hii ni ishara dhabiti kuwa mwanamke ana mimba.

Kuchukia chakula fulani. Unapotunga mimba, huenda ukapata kuwa unachukia aina fulani ya chakula. Kunusa baadhi ya chakula huenda kutakufanya uhisi kutapika. Hii ni njia ya kufahamu kuwa una mimba.

Kifunga choo. Hali ya kufunga choo husababishwa na kubadilika kwa viwango vya homoni mwilini. Ongezeko la homoni mwilini hupunguza utaratibu wa kuchakata chakula mwilini.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Ni Nini Cha Kutarajia Katika Miezi Sita Ya Ujauzito

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Ukuaji Wa Fetusi Na Dalili Za Mimba Ya Mwezi Mmoja
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it