Kwa kawaida, wataalum wa afya huhesabu wiki ya kwanza ya ujauzito kutoka siku ya kwanza ya hedhi ya mzunguko wa mwisho ya mwanamke. Hata iwapo mwanamke hana mimba katika wakati huu. Ni vigumu kudhibiti dalili za mimba ya siku moja, kwani huenda zikawa ni dalili za PMS. Kuhesabu wiki ya kwanza ya mimba kutoka mzunguko wa mwisho wa mwanamke kunasaidia kubaini siku ambapo mwanamke anatarajia kujifungua. Tuna angazia dalili za mimba ya wiki moja.
Dalili za mimba ya wiki moja: Dalili za mapema katika mimba

Baadhi ya wanawake wanaweza kuhisi maumivu ya tumbo yai linapojipandikiza kwenye ukuta wa uterasi. Wanawake wanaweza kuhisi maumivu kwenye tumbo ya chini, sehemu ya pelviki ama kuumwa na mgongo. Maumivu haya huisha baada ya siku chache na sio wanawake wote wanaohisi uchungu huu.

Kuvuja damu ni dalili ya mapema ya mimba. Damu ya implantation ama kupandikiza kwa yai huwa tofauti na damu ya kawaida. Damu hii huwa nyepesi, matone machache ya damu ya pinki ambayo huisha baada ya masaa ama siku chache.
Ishara zaidi za mapema katika mimba
Ishara za mimba za wiki moja huwa tofauti kwa kila mwanamke.
- Kichefuchefu
- Kutapika mara kwa mara
- Kuenda haja ndogo mara nyingi
- Kuumwa na kichwa
- Kujaa gesi tumboni
- Uchovu
- Mhemko wa hisia
- Kutamani na kuchukia vyakula fulani
- Kuumwa na tumbo
- Mabadiliko kwenye maziwa, kufura, kuuma ama kuongezeka kwa saizi
Kufanya kipimo cha mimba
Kipimo cha mimba kinapima kuwepo kwa kichocheo cha mimba kinachofahamika kama Human Chorionic Gonadotropin (hCG). Huonekana tu, mwanamke anapokuwa na ujauzito. Mwanamke anayepanga uzazi anashauriwa kufanya kipimo cha mimba punde tu baada ya kukosa hedhi yake. Kuna kiwango cha wanawake ambacho huwa na viwango vya chini vya homoni hii na huenda ikachukua muda kwa viwango vyake kuonekana kwenye kipimo cha mimba. Ili kupata matokeo bora, mwanamke anapaswa kufanya kipimo cha mimba baada ya kukosa kipindi cha hedhi. Na kufanya kipimo hiki, muda tu baada ya kuamka kabla ya kunywa chochote.
Hitimisho
Dalili za mimba huwa tofauti kwa kila mama. Huku wengine wakifahamu dalili za mimba ya siku moja, wengine huchukua muda kabla ya kuona dalili zozote. Dalili kama maumivu ya kichwa, kuvuja damu na kuhisi uchovu huwa maarufu zaidi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Ishara Na Mabadiliko Yanayofanyika Mwilini Katika Mimba Ya Miezi Mitatu Mapacha