Jinsi Ya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba (Dalili Za Mwanzo Za Mimba)

Jinsi Ya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba (Dalili Za Mwanzo Za Mimba)

Kuhisi uchovu ni mojawapo ya dalili za mwanzo za mimba. Mwanamke akiwa na mimba, mwili hutoa kiwango kikubwa cha homoni ya progesterone.

Je, una shaka kuwa huenda ukawa na ujauzito? Njia haswa ya kudhabiti endapo una mimba ni kwa kufanya kipimo cha kudhihirisha hali yako ya mimba. Matokeo hasi ama chanya. Ila, kwa kuangazia dalili za mwanzo za mimba, una weza fahamu kama una tarajia mtoto.

Dalili za mimba huwa sawa kwa wanawake wote?

Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya wanawake kwani kila mtu ni tofauti. Vivyo hivyo, ishara za mimba kwa mwanamke aliye kuwa na mimba hapo awali zina tofautiana.

Dalili za mimba zina karibiana sana na zile za wakati wa hedhi ya mwezi ya mwanamke. Kwa hivyo kuwa makini ili uweze kutofautisha kati ya hizi. Tuna dadisi zaidi kuhusu ishara za mwanzo za mimba.

Dalili za mwanzo za mimba

Maumivu ya tumbo 

dalili za mwanzo za mimba

Baada ya kupevushwa na manii, yai lililo rutubishwa hujipandikiza kwenye uterasi ya mama. Mama ataanza kushuhudia maumivu ya tumbo ya mji wa mimba ama kutokwa na matone ya damu. Damu hii hutokana na kupandikiza kwa yai kwenye mji wa mimba. Ishara inayo shuhudiwa siku 12 hadi 14 baada ya yai kurutubishwa, ama baada ya tendo la ndoa.

Maumivu ya tumbo ni sawa na uchungu ambao mwanamke hushuhudia anapo karibia kuanza kipindi chake cha hedhi.

Kuhisi kichefuchefu

kutapika katika mimba

Hii ni mojawapo ya ishara maarufu zaidi ya ujauzito. Mabadiliko katika viwango vya homoni mwilini vinachangia pakubwa katika mwanamke kuhisi kichefuchefu anapokuwa na mimba.

Kuumwa na chuchu za matiti

matiti kuuma husababishwa na nini

Baada ya kupevuka kwa yai, kiwango cha homoni mwilini hubadilika. Mabadiliko haya yatabadilisha matiti na kuyafanya yajae. Wiki mbili baada ya kurutubishwa kwa yai, mwanamke ataanza kuhisi kana kwamba chuchu zimefura ama zina vidonda. Pia, chuchu ambazo huwa nyeusi huwa nyeusi zaidi.

Mwanamke akiwa na vipindi vya hedhi ama anapo karibia kuwa nazo, huenda akihisi kana kwamba chuchu zina uma.

Kuhisi uchovu mwingi

dalili za mwanzo za mimba

Kuhisi uchovu ni mojawapo ya dalili za mwanzo za mimba zinazo fahamika sana. Mwanamke akiwa na mimba, mwili hutoa kiwango kikubwa cha homoni ya progesterone. Inayo sababisha mwanamke kuhisi uchovu wakati wote.

Soma Pia: Aina Mbili Kuu Za Vipima Mimba Vilivyoko!

Written by

Risper Nyakio