Je, dalili za saratani ya matiti ni zipi? Kufahamu jinsi ambavyo maziwa yako hukaa kwa kawaida ni muhimu katika afya yako ya maziwa. Kufanya vipimo vya mara kwa mara vya saratani ni muhimu na kila mtu anapaswa kuratibisha vipimo hivi. Kufahamu jinsi ambavyo maziwa yako hukaa na kuhisi kwa kawaida kutafanya iwe rahisi kugundua kunapokuwa na mabadiliko mepesi mwilini.
Dalili za saratani ya matiti

Ishara ya kwanza na iliyo maarufu zaidi ya saratani ya matiti ni uvimbe kwenye titi. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa sio uvimbe wote unaodhihirisha saratani ya matiti. Dalili za saratani ya matiti huchukua muda kabla ya kuanza kuonekana na pia hakuna maumivu.
- Uvimbe kwenye titi ama kwenye kwapa
- Titi kubadili umbo ama shepu na kuwa kubwa zaidi
- Chuchu kutoa maji, usaha ama damu
- Rangi ya titi kubadili na kuwa rangi la chungwa
Mambo yanayoongeza nafasi ya kupata saratani ya ziwa

Jinsia. Wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa saratani ya matiti.
Hedhi. Wanadada wanaoanza vipindi vya hedhi mapema maishani wangali wachanga wako katika hatari zaidi ya kupata saratani ya ziwa.
Kunyonyesha. Wanawake wanaokosa kunyonyesha baada ya kujifungua ama wanaonyonyesha kwa muda mfupi wana nafasi zaidi za kutatizika kutoka na ugonjwa huu.
Ufuta kwenye chakula. Lishe hafifu kama iliyo na mafuta mengi inamweka mama katika hatari ya kupata saratani ya ziwa.
Pombe. Watu wanaotumia pombe zaidi wanaweza pata saratani kwa urahisi ikilinganishwa na wasio tumia pombe.
Uvutaji wa sigara. Walio na uraibu wa kuvuta sigara wanaongeza nafasi zao za kupata saratani.
Kutofanya mazoezi. Mazoezi yana manufaa mengi kwa mwili. Watu wasiofanya mazoezi kamwe maishani mwao wanahatarisha maisha yao. Hawatoi sumu zilizoko mwilini na huenda zikasababisha chembechembe zinazogeuka kuwa saratani.
Uzito uliopindukia. Watu walio na uzito mwingi wa mwili wana nafasi zaidi ya kuugua maradhi haya, ikilinganishwa na watu wenye uzito wa wastani.
Jinsi ya kujilinda dhidi ya kupata saratani ya ziwa
- Kufanya screening ama vipimo vya ziwa kila mwaka
- Kujichunguza mara kwa mara kuhakikisha kila kitu kiko shwari
- Kufanya mazoezi mara kwa mara
- Kuangalia uzito wako wa mwili
- Kuzingatia ulaji wa lishe bora
Soma Pia: Sababu Kwa Nini Chuchu Zako Zinauma Zisizo Husika Na Saratani