Maarifa ya dalili za siku za hatari na siku za hatari zinamsaidia mwanamke anapofanya uamuzi wa kuwa mzazi. Siku ya kupevuka kwa yai ama ovulation huwa tofauti kwa kila mwanamke. Kufahamu siku ya ovulation kunamsaidia mwanamke kujua siku zake za hatari, ikiwa angependa kupata mimba, wakati mzuri wa kufanya tendo la ndoa. Kwa wasio tayari kuwa wazazi, kufahamu siku hizi kunawasaidia kujitenga na tendo na ndoa hadi wanapokuwa katika siku salama.
Tazama yanayotendeka katika siku ya ovulation, dalili za ovulation na siku za kupevuka kwa yai.
Kuengua Kwa Yai

Kuengua kwa yai ni nini?
Hii ni hatua katika mzunguko wa hedhi wa mwanamke ambapo, yai lililokua linaachiliwa kutoka kwa ovari. Na kuwa chanzo cha utaratibu wa kurutubishwa. Mwanamke anapozaliwa, huwa na mamilioni ya mayai yasiyokomaa, yanayongoja kukomaa kisha kuachiliwa kutoka kwa ovari. Kila mwezi, yai moja lililokua huachiliwa kutoka kwa ovari ya mwanamke. Kisha kusafiri kwenye mirija ya uzazi. Yai linapokutana na manii ya mwanamme, linarutubishwa na mchakato wa kutengeneza mtoto kuanza.
Siku za ovulation
Mzunguko wa hedhi wa kawaida huwa siku 28, lakini kuna walio na siku chache zaidi 21, na wengine hadi 32. Kila mwanamke huwa na mzunguko tofauti, ni muhimu kuelewa mzunguko wake. Njia rahisi ni kuhesabu siku kutoka siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi, hadi siku ambapo kipindi kifuatacho kitaanza. Kwa wanawake walio na mzunguko wa siku 28, siku ya ovulation huwa siku ya 14. Walio na mzunguko wa siku 21, siku ya kupevuka kwa yai huwa siku ya 7, huku wenye mzunguko wa siku 35, siku ya kupevuka kwa yai ikiwa siku ya 21.
Kuna uwezekano wa siku ya ovulation kukosa kuwa ya kawaida kwa baadhi ya wanawake. Kama vipindi vyao vya hedhi sio vya kawaida, bila shaka siku ya kupevuka kwa yai itabadilika pia.
Kipindi cha kupevuka kwa yai

Tofauti na manii ya mwanamme ambayo huwa na uwezo wa kuishi kwa muda wa siku 5, yai la mwanamke hubaki kwa siku moja. Kwa hivyo, kufanya mapenzi siku 5 ama 3 kabla ya siku ya ovulation, kunaongeza nafasi za mama kushika mimba.
Dalili za siku za hatari
- Uwezo ulioongezeka wa kunusa
Kwa baadhi ya wanawake, uwezo wa kunusa vitu ikilinganishwa na siku za kawaida huwa ishara kuwa ako katika siku zake za rutuba.
- Matiti kuwa nyororo ama kuuma
Mabadiliko haya husababishwa na ongezeko la homoni mwilini kabla ya siku ya ovulation kufika. Mabadiliko haya huenda yakawa kabla ama baada ya siku ya ovulation.
- Kuumwa na sehemu ya chini ya tumbo
Kwa baadhi ya wanawake wanaohisi siku ya ovulation inapo anza, dalili kuu huwa kuhisi maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo zao. Uchungu huu huwa upande wa ovari inayoachilia yai.
- Mabadiliko ya uchafu ukeni
Mwanamke anapokaribia siku ya kuengua kwa yai, mwili hutoa viwango zaidi vya kichocheo cha estrogen na kufanya uchafu ukeni uongezeke kwa kiwango na uwe mwepesi zaidi. Rangi yake ni ya sehemu nyeupe ya yai.
Wanawake wanapokaribia siku ya ovulation, wao hushuhudia ongezeko la hamu ya mapenzi. Ikiwa mwanamke hataki kupata mimba, ni muhimu kujtenga na kufanya tendo la ndoa katika kipindi hiki ama kutumia mbinu mojawapo ya kupanga uzazi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Ongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Kwa Kutumia Kalenda Ya Ovulation