Je, nitaanza kuhisi dalili za uja uzito mwilini mwangu lini?

Je, nitaanza kuhisi dalili za uja uzito mwilini mwangu lini?

Mwana dada anapo kuwa makini, ni rahisi kujua anapo kuwa mja mzito. Hii ni kwa sababu muda tu anapo tunga mimba, mwili huanza kutoa ishara mbali mbali. Kama vile uchovu na kuhisi kutapika.

Mwili wako utaanza kukutumia ishara kuwa una mimba muda mfupi baada ya kutunga mimba. Kinacho leta utata ni kutofautisha iwapo dalili hizi ni ishara ya uja uzito ama hedhi. Hii ni kwa sababu dalili hizi za uja uzito na hedhi ni sawa. Ishara za uja uzito huanza kuonekana wakati unapo tarajia kipindi chako cha kila mwezi. Ila hautapata hedhi mwezi huo. Kujua iwapo ni dalili za uja uzito ama za hedhi itakusaidia kujua ama ni wakati mwema wa kuzificha glasi za divai na kuanza kununua vitu vya mtoto unaye mtarajia.

 

Dalili za mapema za uja uzito ni tofauti kwa kila mmoja. Wanawake wengine huanza kuskia ishara za uja uzito wiki moja ama mbili baada ya kutunga mimba. Iwapo wengine hawaskii tofauti yeyote kwa miezi kadha.

 

Kwa somo katika mada hii, wanawake 136 waliokua wakijaribu kupata mimba walieka rekodi za kila siku za dalili kutoka wakati walipo acha kutumia dhibiti za kuzaliwa hadi walipokuwa wiki 8 katika mimba. Hiyo ni kuhesabu wiki nane kutoka siku ya mwisho walipopata hedhi. Matokeo walikuwa:

 • Asilimia 50 walikua na dalili za uja uzito walipokuwa wiki 5 katika mimba.
 • Asilimia 70 walipata ishara katika wiki ya sita.
 • Asilimia 90 walipata ishara katika wiki ya nane.

 

Vile Dalili za Uja Uzito Zinavo Anza

Dalili iliyo dhahiri zaidi ya uja uzito ni kukosa kupata hedhi. Ila mbele ya hilo, mwili wako ulikua umeanza kujitayarisha kwa muda wa angalau wiki mbili. Baadhi ya dalili za mapema za uja uzito zinaweza anza siku sita baada ya kutunga mimba. Mwili wako huanza kujitayarisha kwa mimba punde baada ya yai la mwana mke na mbegu ya mwanamme kuungana. Baadhi ya madaliko haya huchangikia katika mabadiliko ya kimwili. Idadi ya homoni inapo ongezeka mwilini, ni sababu unapo anza kuskia mabadiliko haya.

 

Nini haswa unacho stahili kuangalia kwa hizo wiki chache za mwanzo baada ya kuitunga mimba? Wanawake wengi wanasemekana kuskia tofauti. Unaweza fikiria mambo unayo yaskia ni kufuatia majira yako ya hedhi mpaka unapo tambua kuwa dalili hizi ni tofauti na unazo shuhudiwa kila mwezi. Mabadiliko unayo shuhudiwa hukua machache na unaweza kuyapuuza ilhali ni muhimu kuyatilia mkazo yanapo ongezeka.

Mambo machache yanayo tendeka hapa ni: kushuhudia damu iliyo nyepesi kuliko ya majira ya hedhi, uchungu tumboni kwa muda wa siku 6-12 baada ya kuitunga mimba. Matiti kuwa tefu na uchungu wakati mwengine wiki moja ama mbili baada ya kutunga mimba. Kuhisi uchovu wiki moja baada ya kutunga mimba, kuhisi kutapika na kuchagua chakula kutoka wiki ya pili baada ya kutunga mimba.

 

 

 

 

Ishara na Dalili Muda (kutoka alipokosa majira yake ya hedhi)
Maumivu kidogo kwa tumbo na kushuhudia damu Wiki 1-4
Kutopata majira ya hedhi Wiki 4
Uchovu Wiki 4-5
Kuhisi kutapika Wiki 4-6
Maumivu kwa matiti Wiki 4-6
Kukojoa ovyo ovyo Wiki 4-6
Kufura tumbo Wiki 4-6
Ugonjwa wa mwendo Wiki 5-6
Mhemko wa hisia Wiki 6
Mabadiliko ya joto mwilini Wiki 6
Shinikizo la damu Wiki 8
Uchovu mwingi na kiungulia Wiki 9
Mapigo ya juu ya moyo Wiki 8 – 10
Matiti na chuchu kubadilika Wiki 11
Chunusi Wiki 11
Ongezeko la kilo mwilini Wiki 11
Mwanga wa uja uzito Wiki 12

 

 

Dalili zilizo wazi kabisa za kuwa mwangalifu ni kuhisi kutapika, kichefuchefu, uchovu, kukojoa ovyo na chunusi na matiti kuvimba. Ishara hizi zaweza kuwa kidogo ama kwa wingi. Kipimo ka uja uzito ni njia hakika ya kudhibitisha iwapo una mimba. Kipimo cha nyumbani hufanya kazi wiki moja baada ya kukosa kupata majira yako ya mwezi.

 

Dalili Zingine Unazo Weza Kushuhudia Katika Wiki Ya Nane Ni:

 • Uchungu kidogo na usumbufu (bila ya damu)
 • Kufura tumbo
 • Kuvimbiwa
 • Kiungulia
 • Msongamano wa pua
 • Kukosa hewa
 • Mtamanio wa chakula ama kuziepuka
 • Kuhisi kuumwa na kichwa kwa umbali
 • Mishipa kushikana
 • Kuhisi kujikuna viganjani vya mikono
 • Kuwa na ngozi nyeusi (usoni, mwili wa chini, tumbo)

 

Njia Za Kupambana Na Dalili Zako Za Mimba

 • Epukana na kuvuta sigara, kunywa pombe ama dawa za kulevya.
 • Iwapo una kunywa dawa, uliza Daktari wapo iwapo zita kuwa na adhari yeyote kwa mtoto aliye tumboni.
 • Wiki za mwanzo za uja uzito zitakufanya usiskie uchovu na kulegea. Dhibitisha Unapata usingizi wa kutosha.
 • Kupaweka mahali pako pa malezi pakiwa pamepoa. Viwango vya joto mwilini vinaweza kua juu wiki za kwanza za uja uzito.
 • Nunua sindiria nzuri za pamba isiyo na waya kupunguza chunusi.
 • Viweke vitamu tamu vya chumvi karibu na kitanda chako kukabiliana na gonjwa la asubuhi.
 • Kunywa maji kwa wingi.
 • Mfahamishe Daktari wako iwapo huezi eka ugiligili ama vyakula chini.
 • Nunua pedi za matiti zinazo toshea kwa sindiria yako kupunguza msuguano kwa chuchu zako na uchungu kwa chuchu.
 • Kunywa angalau 300 mL ya ugiligili zaidi- angalau kikombe kimoja.
 • Panga safari zako za msalani muda kabla unapoenda.
 • Fanya mazoezi yaliyo salama kwa uja uzito iwapo bado hujaanza.
 • Jifunze kuangalia shinikizo lako la damu mara kwa mara.
 • Uliza daktari wako kuhusu mpango wa chakula wa kibinafsi ili kusaidia kupunguza shinikizo la damu.

 

Wataalamu wana bashiri kuwa ishara hizi, hata kama hazipendezi zina changia kusudi muhimu iwapo zina linda wana wake kuto vila vyakula ambavyo vina weza kumwumiza mtoto anaye kua tumboni la mama anapo kua. Pia zina weza mtahadharisha mama kuhusu hali yao ya uja uzito na kuwasaidia kufanya mabadiliko ya mitindo ya maisha na kutafuta utunzaji wa ujauzito.

 

Walakini, kwa sababu ishara za mapema zaidi hazianzi mpaka baada ya kiinitete kinapo anza kuumbika. Jifanye unaweza kuwa mja mzito na kujichunga ipasavyo, hata kabla ya kuzishuhudia ishara na dalili ama kupata kipimo chanya za uja uzito. 

Read Also: 5 Recipes Your Kids Will Love Snacking On

 

 

 

Written by

Risper Nyakio