Dalili za mapema za ujauzito zinamsaidia mwanamke kufahamu iwapo anatarajia kuwa mama. Na kumwezesha kuanza kliniki za ujauzito mapema iwezekanavyo. Wakati ambapo kuzingatia ishara za mapema za mimba ni vyema, ni muhimu kukumbuka kuwa ishara za ujauzito huenda zikawa sawa na ishara za hedhi kukaribia. Mwanamke anaposhuku kuwa ana mimba ni vyema kufanyiwa ultrasound na kipimo cha mimba kudhibitisha hali yake.
Dalili za Ujauzito
Wiki ya mwisho ya ujauzito inafahamika kama wiki ya kwanza ya ujauzito. Dalili za mapema za ujauzito ni:
- Maumivu ya tumbo na kuvuja damu

Katika wiki ya nne ya ujauzito, yai hujipandikiza kwenye kuta za uterasi na kufanya mwanamke apate implantation bleeding. Kwa mama asiye makini, huenda akadhania hii ni damu ya hedhi, hata kama ni tofauti sana. Ni nyepesi na pia rangi yake ni ya nyekundu, pinki ama ya hudhurungi.
Mwanamke anapogundua kuwa ana damu ya implantation anapaswa kujitenga na utumiaji wa vileo, sigara na dawa za kulevya.
2. Kukosa kipindi cha hedhi
Yai linapomaliza kujipandikiza, mwili wa mwanamke huanza kutoa kichocheo cha human chorionic gonadotropin (hCG). Homoni hii inafahamika kama homoni ya mimba na inausaidia mwili kudumisha ujauzito. Homoni hii inapotolewa mwilini, mwanamke hukosa kipindi chake cha hedhi, inakomesha utoaji wa mayai yaliyokomaa kutoka kwa ovari.
Mwanamke anapokosa hedhi, anapaswa kufanya kipimo cha hedhi kudhibitisha iwapo ana mimba. Kuwasiliana na daktari wake kuratibisha kufanyiwa kipimo na kupatiwa ushauri wa kabla ya kujifungua (prenatal).
3. Uchovu mwingi hata baada ya kuamka

Mwanamke huanza kuhisi kuchoka ovyo ovyo wakati wowote katika safari yake ya ujauzito. Chanzo kikuu ni ongezeko la viwango vya progesterone mwilini na kumfanya kuhisi kulala wakati wote. Mwanamke anastahili kuhakikisha anapata usingizi tosha na kuhakikisha chumba chake cha kulala kina starehe tosha kumwezesha kulala vizuri.
4. Mabadiliko kwenye maziwa
Mabadiliko kwenye maziwa hufanyika baada ya wiki nne. Mwanamke huhisi kuwa chuchu zake zimefura kufuatia ongezeko la homoni mwilini. Huanza kuhisi uchungu kwenye chuchu katika wiki ya 11 ya ujauzito huku rangi yake ikikolea zaidi. Ili kuwa na kipindi rahisi wakati huu, anaweza kuvalia sindiria za pamba kwani zina starehe zaidi.
5. Mhemko wa hisia katika mimba
Ongezeko la vichocheo vya progesterone na estrogene katika ujauzito vinaathiri mhemko wa hisia wa mwanamke. Na kumfanya awe na hisia zaidi kuliko ilivyo kawaida yake. Huenda akahisi ana furaha zaidi, kusombwa na mawazo zaidi, shaka ama kukosa kutulia.
Mwanamke anaposhuhudia dalili za ujauzito tulizoangazia, ni muhimu kuwasiliana na daktari ili aanze kliniki za ujauzito na kuchukua vitamini za prenatals.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Ukuaji Na Maendeleo Ya Fetusi: Mama, Tarajia Haya Katika Mimba Ya Miezi 6