Kuelewa kilicho kawaida katika hedhi na wakati wa kipindi chako cha hedhi kutakusaidia kujua unapokuwa na damu ya hedhi nyepesi. Mwanamke hushuhudia kipindi cha hedhi wakati ambapo kuta za uterasi humwagika baada ya yai kukosa kujipandikiza kupitia kwa mlango wa uke na kizazi chake, kila mwezi.
Mzunguko wa hedhi wa kawaida huwa siku 28, ila kila mwanamke ni tofauti na kipindi hiki huenda kikawa kati ya siku 21 na 31. Kila kipindi cha hedhi huenda kikadumu kati ya siku 3 hadi 7.
Ishara za kukutia kiwewe za hedhi

- Kuvuja damu siku chache zaidi ya mbili
- Kuvuja damu nyepesi sana, isiyo jaza pedi
- Kukosa hedhi kwa mwezi mmoja ama miwili
Ni kawaida kuwa na kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida mara moja ama mbili, lakini ni vyema kuwasiliana na daktari wako. Huenda ukawa na magonjwa fiche na kuyajua kutakusaidia kuya tibu mapema.
Vyanzo za damu ya hedhi nyepesi
Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikamfanya mwanamke kuwa na kipindi cha hedhi chepesi. Kama vile:
Kipindi chako cha hedhi kina weza tofautiana na siku unazo pata hedhi na ikiwa umeanza kupata medhi tu. Ikiwa uko katika umri wako wa ugumba, huenda ukawa na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na vilivyo na damu nyepesi. Mara nyingi, tofauti hii inasababishwa na mabadiliko ya homoni mwilini.
Mbinu tofauti za kupanga uzazi hasa zilizo na homoni huenda zikaathiri hedhi ya mwanamke. Mbinu za kudhibiti uzalishaji kama kutumia tembe, pete na sindano ya miezi mitatu. Baadhi ya mbinu hizi za kupanga uzazi huenda zikafanya mwanamke akose kupata kipindi chake cha hedhi.
Ukigundua kuwa vipindi vyako vya hedhi sio sawa ama umevikosa kwa miezi kadhaa, ni vyema kutafuta mbinu tofauti ya kupanga uzazi.

Uzani wa mwili wako una weza kuathiri kipindi chako cha hedhi. Mwanamke anapokuwa na uzito mdogo ama mwingi wa mwili, huenda kipindi chake kika athiriwa kwa sababu homoni zake hazifanyi kazi inavyo stahili.
Mwanamke anapokuwa na fikira nyingi, ni kawaida kwa akili yake kubadili homoni zake za kipindi cha hedhi. Huenda ukashuhudia vipindi vya hedhi vilivyo na damu nyepesi na kurejelea kipindi cha kawaida baada ya kipindi hicho kigumu kupita.
Kuna sababu nyingi zinazo mfanya mwanamme kuwa na damu ya hedhi iliyo nyepesi. Magonjwa kama PCOS, kufanya mazoezi zaidi ama kula isivyo faa. Wasiliana na daktari wako tatizo hili linapo zidi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Njia Za Kuanzisha Kipindi Cha Hedhi Kinapo Chelewa