Hali ya Amenorrhoea ni pale ambapo mwanamke aliyefikisha umri wa kuanza kupata vipindi vya hedhi hushindwa kupata hedhi. Huenda pia akakosa kupata kipindi chake kwa muda ama kikapitiliza siku. Jambo linalomjaza wasiwasi mwingi. Hali hii inaweza kutokea katika umri wowote maishani mwa mwanamke. Kuna sababu tofauti zinazo mfanya mwanamke kutatizika na hali hii. Je, kuna dawa ya kufungua hedhi? Tuna angazia zaidi.
Vyanzo vya hedhi kuchelewa

Wanawake wengi walio na uzani wa chini kuliko wanavyopaswa, mara nyingi hutatizika na hedhi kuchelewa. Na pia kuwa na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida.
Kuwa na mawazo mengi huathiri utoaji wa homoni muhimu zinazo husika na vipindi vya hedhi.
Mazoezi huwa na faida nyingi kwa mwili, ila unapo pitiliza kiasi cha mazoezi unachofaa kufanya, huwa na athari hasi kwa mwili. Mazoezi makali huathiri homoni mwili na kupunguza kiwango kinachotolewa mwilini. Homoni zisipokuwa sawa mwilini, ni vigumu kwa kazi mwilini kutendeka kama ilivyo kawaida.
Kuna baadhi ya magonjwa yanayo waathiri wanawake kama vile polycystic ovarian syndrome yanayo mfanya mwanamke kutatizika kupata vipindi vyake vya hedhi kama ilivyo kawaida.
Dalili za hali hii
- Kuongeza uzani mwingi kwa kasi
- Kutatizika kupata usingizi
- Kutokuwa na vipindi vya kawaida vya hedhi
- Kuwa na uke mkavu
- Mhemko wa hisia usio wa kawaida
Suluhu la hali hii

- Kuna dawa ya kufungua hedhi iliyo spesheli na inayopatikana kwenye mahospitali. Wakati wote mwanamke anapogundua kuwa ana matatizo ya kuchelewa kwa hedhi, anastahili kuwasiliana na daktari. Mbali na njia hii, kuna mambo ambayo mwanamke anaweza kufanya ili kuboresha afya yake na kupunguza nafasi za hedhi yake kuchelewa.
- Zingatia lishe bora. Chakula ni muhimu katika kusawasisha homoni mwilini. Hakikisha kuwa unakula chakula kutoka kwa kila kundi kisha kuambatanisha na mboga, matunda na maji ya kutosha. Punguza ulaji wa vitamu tamu visivyo kuwa na faida zozote mwilini.
- Ongeza tikiti maji na maziwa ya soy kwenye lishe yako.
Ni vyema kusuluhisha hali hii punde tu mwanamke anapogundua kuwa ana tatizo. Kuchelewa kulitatua huenda kukamfanya augue saratani ya matiti, kukosa hamu ya kufanya mapenzi, kuhisi uchungu mwingi na kuvuja damu baada ya kitendo cha ndoa. Kwani mwanamke ana uke mkavu.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vidokezo 5 Vya Kuwa Na Ujauzito Salama Na Wenye Afya