Kusafisha kizazi ni utaratibu muhimu kuuandaa mwili kushika mimba. Mji wa uzazi una ukuta wa nje, ukuta wa kati na kuta za misuli ama endometrium zilizo ndani ya myometrium ama kuta ya kati. Mwanamke anapokuwa na kipindi chake cha hedhi, kuta za endometrium ndizo huyeyuka na kuvuja damu. Kuna baadhi ya njia na dawa ya kutoa uchafu kwenye kizazi.
Vyanzo vya matatizo kwenye kizazi

Kizazi chenye afya hutengeneza mazingira mazuri yatakayofaa ukuaji na maendeleo ya mtoto. Ili kizazi kuwa na afya, kuna vichocheo vingi vinavyofanya kazi kwa pamoja kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari kwenye kizazi. Kitu chochote kinacho vuruga mpangilio huu hufanya iwe vigumu kwa mwanamke kutunga mimba. Tazama baadhi ya sababu zinazo sababisha kuvurugika kwa afya ya kizazi cha mwanamke.
Mazoezi ni muhimu katika kuwa na afya bora na kuboresha mzunguko wa damu mwilini. Kwa wanawake wasio fanya mazoezi ya aina yoyote, wanapunguza mzunguko wa damu mwilini. Kukaa chini pahali pamoja kwa muda mrefu bila kufanya chochote kunamweka mwanamke katika hatari ya kupunguza nguvu za misuli za kizazi zinazo hifadhi mimba. Ni vyema kwa mwanamke kufanya mazoezi mara kwa mara.
Uvimbe wa aina hii hupatikana kwenye kuta za mji wa uzazi na mwanamke kuhisi uchungu mwingi katika kipindi chake cha hedhi. Kuwa na kipindi cha hedhi chenye uchungu mwingi na kinacho dumu muda mrefu ni baadhi ya ishara za kuwa na fibroids. Ni vyema kupata matibabu na kuwa makini na lishe yako.
- Viwango vya vichocheo kubadilika mwilini
Homoni huchangia pakuu katika utendaji kazi kwenye kizazi. Viwango vya vichocheo hivi visipokuwa sawa, mwanamke ako katika hatari ya kuugua kutokana na fibroids ama endometriosis. Mwanamke anapokuwa na kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida, kupata hedhi nzito na ya muda mrefu na kuumwa zaidi wakati wa hedhi, anapaswa kufanyiwa vipimo. Hizi ni ishara kuwa viwango vya homoni mwilini mwake.
Kuboresha afya ya kizazi

- Kufanya mazoezi. Hatua ya kwanza na iliyo muhimu katika kusafisha kizazi chako. Anza kwa kufanya mazoezi mepesi ili kuimarisha mzunguko wa damu mwilini.
- Kufanyiwa usafishaji wa uzalishaji. Ni njia nyingine ya kusafisha kizazi na kusawasisha viwango vya homoni mwilini. Daktari atakupatia dawa ya kutoa uchafu kwenye kizazi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Lishe Ni Nini Na Inapaswa Kuwa Na Vyakula Vipi Bora Kwa Afya?