Je, kuna dawa ya saratani? Utafiti katika nyanja ya Sayansi unaozidi kufanyika bado haujadhibitisha kinga ya saratani. Hata hivyo, kuna mabadiliko ya kimaisha ambayo mwanamke anaweza kufanya ili kupunguza nafasi za kupata ugonjwa wa saratani.
Dawa Ya Saratani Kwa Kubadili Mfumo Wa Maisha

Sukari hata ingawa inatumika kwa sana, ina athari hasi mwilini. Ina changia pakubwa katika kuongezeka kwa uzito mkubwa wa mwili na ukuaji wa kitambi. Watu zaidi ya bilioni 6 duniani kote wana athiriwa na kisukari. Sukari inachangia katika ukuaji wa haraka wa seli za saratani. Ni vyema kujitenga na utumiaji wa sukari zaidi, pamoja na vyakula vyenye wanga. Kwa mbadala, tumia asali.

Kuna baadhi ya saratani zinazo sababishwa na lishe duni inayo athiri mfumo wa afya. Na kuufanya mwili ukose kinga tosha kujilinda dhidi ya maambukizi na magonjwa. Ni vyema kuhakikisha kuwa unakula lishe bora iliyo na vikundi vyote vya chakula. Hakikisha kuwa lishe yako ina matunda na mboga wakati wote. Pia, punguza ulaji wa protini zinazo tokana na nyama nyekundu. Badala yake, kula protini zinazo tokana na mimea, nyama nyeupe, na njugu. Parachichi ni chanzo bora cha ufuta.

Mazoezi ni muhimu katika kuimarisha kinga mwilini. Kufanya mazoezi siku tatu kwa wiki kunaimarisha afya na kuboresha kinga ya mwili kuweza kupambana na seli za kansa mwilini. Mazoezi husaidia kwa kupunguza kiasi cha insulin kinachotolewa mwilini na kufanya mazingira yasiwe bora kwa ukuaji wa seli zinazo sababisha saratani.

Kulingana na wataalum wa afya, kila mtu anafaa kupata angalau masaa manane ya usingizi kwa siku. Kulala vya kutosha kunasaidia kulinda dhidi ya saratani. Punguza utumiaji wa vitu vyenye miale ama mionzi kama vile rununu ama televisheni. Mazingira bora ni muhimu, jitenge na mazingira yaliyo na kemikali. Zinachangia pakubwa katika kupata kansa.
Mimea bora katika kutatua hali ya kansa
Mmea wa Ginseng, muhimu katika kuongeza kiwango cha seli zinazo pambana na saratani mwilini. Unasaidia katika uponaji wa vidonda mwilini.
Garnoderma, mmea unaosaidia kuboresha kinga mwilini na hivyo basi kuzuia kuugua kansa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kuto Lala Vyema Kuna Kuweka Katika Hatari Ya Kupata Saratani