Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Je, Dawa Za Malaria Zinaweza Kuzuia Mimba?

3 min read
Je, Dawa Za Malaria Zinaweza Kuzuia Mimba?Je, Dawa Za Malaria Zinaweza Kuzuia Mimba?

Athari za malaria kwa ujauzito ni pamoja na: upungufu wa damu(anaemia), kuharibika kwa mimba, moyo wa mtoto kusimama, na kuzaa mtoto njiti.

Malaria ni ugonjwa unaojitokeza kama homa. Huandamana na maumivu katika viungo, kutokwa na jasho, kutetemeka na kutapika. Huletwa  na viini vinavyoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya anopheles wa kike. Ila utafiti haujaonyesha ufanisi wowote kuwa dawa za malaria zinaweza zuia mimba.

Dawa Za Malaria Zinaweza Zuia Mimba?

dawa za malaria zinaweza zuia mimba

Ugonjwa wa malaria ni hatari na huathiri watu wote. Ila ni hatari zaidi kwa watoto wadogo na mama wajawazito. Kwa kina mama wajawazito ni rahisi sana kupata malaria. Pia mtoto aliye tumboni. Hivyo ni vyema kama mtu anajihisi kuwa na dalili za malaria kutembelea zahanati ili kupata dawa. Dawa kama vile Kwinini, clindamycin na zile za mseto  Jamii ya Artemisin hutumika katika kutibu malaria.

Hizi dawa hufanya kazi kwa kupigana na viini vinavyosababisha malaria. Muundo wa kemikali kwenye dawa za malaria ni kutambua na kuua viini vya malaria. Ili mwanamke kubeba mimba, lazima mbegu za uzazi za mwanamume kurutubisha  yai la mwanamke. Hili hufanyika kwenye mirija ya fallopia. Hivyo basi, kuzuia ujauzito lazima uweze kuzuia mbegu za mwanamume kutofikia yai la mwanamke.

Ama pia kuzuia ovari kutoachilia yai ili lisije likapatana na mbegu za mwanamume. Hili hufanyika kwa mwingiliano na homoni. Dawa za malaria hazijaonyesha mwingiliano wowote na homoni za kike. Pia huwa hazina uwezo wowote wa kuua mbegu za uzazi za kiume. Hivyo basi hakuna utafiti tosha wa kuonyesha kuwa dawa za malaria zinaweza zuia mimba.

Kuna njia tofauti za kuzuia mimba:

  • Njia za vizuizi (barrier method) - Hufanya kazi kwa kuzuia mbegu ya uzazi ya kiume kulifikia yai la uzazi la mwanamke. Hizi ni kama vile: kondomu ya kike, kondomu ya kiume na daframu. Njia hizi hutumika kila wakati mwanamke anapofanya ngono. Hizi njia hazibadilishi uwezo wa mwanamke wa kuzaa ama kupata hedhi kila mwaka
  • Njia za homoni - Hizi njia hufanya kazi kwa kuzuia ovari za mwanamke kuachia mayai ya uzazi. Hizi njia ni vijiti, sindano na vidonge vya majira. Mwanamke anaposimamisha matumizi ya njia za homoni ovari zake huanza kuzalisha mayai tena
  • Njia za kitanzi na zile za kudumu kama vile vasektomi na kufunga kizazi
  • Njia asili - Hizi njia hujumuisha kuepuka mwingiliano wa kingono mwanamke anapokuwa kwenye kipindi chake cha rutuba

Hatari Ya Ugonjwa Wa Malaria Kwa Ujauzito

dawa za malaria zinaweza zuia mimba

Ni muhimu wanawake wajawazito kutibiwa malaria haraka wanapokuwa wagonjwa. Dawa za malaria zinaweza kuwa na madhara kwa mama mjamzito. Lakini hakuna ishara kuwa dawa za malaria zinaweza zuia mimba. Wiki kumi na mbili za awamu ya kwanza ya ujauzito, mama atatibiwa kwa kwinini na Clindamycin. Pia  kwinini hutumika pekee iwapo  clindamycin haipatikani.

Athari za malaria kwa ujauzito ni pamoja na: upungufu wa damu(anaemia), kuharibika kwa mimba, moyo wa mtoto kusimama, kuzaa mtoto njiti(low birth weight), malaria kuingia kwenye mfuko wa uzazi (placenta) na kuifanya  ngumu kujua kama mama au mtoto wana malaria, pia mtoto anaweza kufia tumboni.

Kuna njia zinazotambulika na zina ufanisi mkubwa katika kuzuia mimba. Ila hakuna utafiti tosha iwapo dawa za malaria zinaweza  zuia mimba . Kuna uwezekano wa madhara kwa mimba iwapo mama atazitumia wakati wa ujauzito.

Chanzo: healthline

Soma Pia: Mimba Hutokea Vipi? Mchakato Unao Sababisha Mimba Kufanyika

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Je, Dawa Za Malaria Zinaweza Kuzuia Mimba?
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it