Yote Unayo Hitaji Kufahamu Kuhusu Dhiki Baada Ya Kujifungua

Yote Unayo Hitaji Kufahamu Kuhusu Dhiki Baada Ya Kujifungua

Dhiki baada ya kujifungua ni hali iliyo kawaida kwa wamama walio jifungua hasa kwa mara ya kwanza. Moja kati ya mama 7 hutatizika na hali hii.

Baada ya kungoja miezi tisa kumpokea mtoto, watu wengi huenda waka tarajia mama mpya kumkaribisha mtoto wake kwa furaha na shukrani. Huenda hii ikawa sio kesi wakati wote, kwani wamama wengi hutatizika na afya ya kiakili punde tu baada ya kujifungua. Kwa asilimia 11-20 ya wamama wa mara ya kwanza wanao pata dhiki baada ya kujifungua, huenda wakawa na huzuni, kukosa furaha, kuwa na wasiwasi, upweke na uchovu mwingi.

Kwa hivyo dhiki baada ya kujifungua ni nini na huathiri wamama wa mara ya kwanza kivipi?

Dhiki baada ya kujifungua- zaidi ya fikira za mtoto

dhiki baada ya kujifungua

Tofauti na mawazo ya mtoto, fikira nyingi baada ya kujifungua huwa haziishi hivyo tu. Kwa kawaida hutokea kama kufilisika kimawazo, kuwa na wasi wasi mwingi, mhemko wa hisia, uchovu, kukosa furaha na upweke wa kupindukia. Hisia hizi zinaweza onekana wiki ama miezi baada ya kujifungua. Wanawake wanao tatizika na hali hii wata tatizika kufanya kazi zao siku baada ya nyingine.

Cha kuhuzunisha ni kuwa hali ya mama na mtoto ina weza athiriwa kwani mama hushindwa kutekeleza majukumu yake ya kumtunza mtoto anapo kuwa akitatizika bado.

Kulingana na somo lililo chapishwa kwenye makala ya JAMA Psychiatry, moja kati ya wanawake 7 hutatizika na kufilisika kimawazo baada ya kupata mtoto. Somo lili tafiti wanawake 10,000 walio kuwa kati ya wiki 4-6 baada ya kujifungua. Nambari ya wanawake hawa ilialikwa kufanyiwa vipimo vya kiakili baada ya kipimo cha kwanza. Kati ya wanawake 10,000, 1396 wali dhihirisha matokeo chanya ya kufilisika kimawazo baada ya kujifungua.

Hitimisho ya vipimo hivi ilionyesha kuwa asilimia 30 ya wanawake walishuhudia mawazo mengi kabla na baada ya kujifungua. Karibu nusu ya idadi hii walikuwa na tatizo la kuwa na wasiwasi mwingi, hali inayo husishwa na kufilisika kimawazo.

Kuwepo kwingi kwa hali hii kunaonyesha kuwa ni jambo la kutia wasiwasi.

Ishara na dalili za dhiki baada ya kujifungua

dhiki baada ya kujifungua

Kuna uwezekano wa kutatizika na mawazo mengi baada ya kupata mtoto bila kufahamu kuhusu hali hii. Katika mahali ambapo afya ya kiakili hapatiwi kipaombele, visa sugu vya mawazo mengi baada ya kujifungua huenda vikazidi na kubaki kama havija dhibitiwa.

Je, kuna ishara za kuwa makini kuhusu? Ndiyo, sio lazima uangalie kwa makini kuona ishara hizi:

 • Hisia za hatia na kutokuwa na dhamani
 • Kuhisi uwoga wa kuwa mama mbaya
 • Huzuni huku ukilia mara kwa mara
 • Kuhisi usingizi ama kulala sana; kushindwa kulala ama kubaki bila usingizi
 • Kushindwa kukumbuka ama kusahau mambo na vitu
 • Mhemko wa hisia kutoka kwa chuki hadi kwa kukasirika ovyo
 • Hofu ya kubaki peke yako na mtoto
 • Kukosa hamu ya shughuli ambazo hapo awali ulifurahia
 • Wasiwasi mwingi
 • Tatizo la ulaji-kula sana ama kidogo sana
 • Fikira za kuji jeruhi ama mtoto
 • Kuhisi hauna dhamana

Unapaswa kuenda kwa kituo cha afya ikiwa dalili hizi zina dumu zaidi ya wiki 2.

Nani aliye katika hatari ya kupata dhiki baada ya kujifungua?

Yote Unayo Hitaji Kufahamu Kuhusu Dhiki Baada Ya Kujifungua

Sababu zifuatazo 13 zina amua sababu za hatari za ugonjwa huu.

 1. Wanawake walio na historia ya mawazo mengi kabla ya mimba na kujifungua
 2. Mawazo mengi katika mimba
 3. Wasiwasi mwingi katika na kabla ya mimba
 4. Matukio ya kukwaza yanayo tendeka kabla, baada na katika ujauzito na kujifungua
 5. Ndoa zenye changamoto ama uhusiano unao didimia
 6. Dhiki inayo husika na utunzaji wa mtoto
 7. Kukosa watu wa kukuegemeza katika na baada ya mimba
 8. Kukosa kujiamini kwa sababu yoyote hata mimba
 9. Kushindwa kudhibiti mhemko wa mtoto
 10. Umasikini ama kukosa fedha
 11. Wakati ambapo haukuwa umepangia mimba ama haikutarajiwa
 12. Kuwa mama pekee

Kupima mawazo mengi baada ya kujifungua

Wanawake wanao shuhudia dalili za hali hii wanapaswa kuwasiliana na daktari. Ili kupata kipimo halisi, madaktari wata angalia ukubwa wa hali yako kwa kuuliza maswali kuhusu ishara zako ili kuhakikisha sio aina nyingine ya maradhi kama changamoto ya bipolar. Pia kutakuwa na vipimo kuhakikisha kuwa sio hali ya hyperthyroidism.

Baadhi ya matibabu ya hali hii

 • Dawa za kufilisika kimawazo baada ya kujifungua
 • Kutumia antidepressants
 • Vipindi vya therapy

Ukigundua kuwa una hali hii, ni vyema kuwasiliana na daktari ili ufanyiwe vipimo na kuanza matibabu mapema. Hakikisha kuwa unaongea na jamii na marafiki zako. Na kamwe usione aibu kuhusu hali yako.

Vyanzo: JAMA Psychiatry

netdoctor.co.uk, PubMed.gov

Soma Pia: Sababu 6 Kwa Nini Kinya Cha Mara Ya Kwanza Baada Ya Kujifungua Huuma Kuliko Uchungu Wa Uzazi!

Written by

Risper Nyakio