Divai Nyekundu Na Chokleti Zinaweza Saidia Kurekebisha Viwango Vya Homoni Katika Wanawake

Divai Nyekundu Na Chokleti Zinaweza Saidia Kurekebisha Viwango Vya Homoni Katika Wanawake

Kitu kinacho patikana kwenye ngozi ya zabibu na divai nyekundu zinaweza saidia mwanamke kurekebisha na kusawasisha viwango vya homoni mwilini.

Kuna habari njema kwa wanaopenda divai huko nje- kulingana na utafiti uliochapishwa kwenye Makala ya Clinical Endocrinology & Metabolism, kitu kinacho patikana kwenye ngozi ya zabibu na divai nyekundu zinaweza saidia mwanamke kurekebisha na kusawasisha viwango vya homoni mwilini, UPI ili ripoti.

Watafiti hawa kutoka kwa chuo kikuu cha California huko San Diego waligundua kuwa resveratrol inayo patikana kwenye divai nyekundu, zabibu, njugu na chokleti zinaweza saidia kuregesha viwango vya estrogen. Na kusaidia kwa watu walio na tatizo la PCOS polycystic ovary syndrome ambayo ni sababu kuu ya ugumba kwa wanawake.

Je PCOS

divai nyekundu

Wanawake wote wana viwango vidogo vya testosterone na homoni za kiume za ngono lakini wanawake walio na PCOS wana viwango vingi kidogo. Kutokuwa sawa huku kwa viwango vya homoni hufanya baadhi ya wanawake walio na PCOS huwa na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida ama kukosa vipindi vyao. Ishara zingine huwa ongezeko la uzito, acne, nywele zaidi kwenye uso na mwili na ugumba. Isipo tibiwa, PCOS inaweza sababisha hali isiyo tibika kama kisukari ama ugonjwa wa moyo.

Kulingana na WebMD, chanzo cha PCOS hakija dhibitika bado, lakini kuna uhusiano wa geni- ikiwa wanawake kwa familia yenu wanayo, nafasi zako za kuwa nayo ni nyingi.

Matokeo ya utafiti

divai nyekundu

Watafiti waligundua kuwa wanawake 30 walio na PCOS katika utafiti wa miezi mitatu Poland. Waligundua kuwa viwango vya testosterone katika wanawake walio chukua resveratrol ilianguka kwa 23.1%. Lakini walio chukua placebo walikuwa na ongezeko la 2.9 katika viwango vya testosterone.

Pia, waligundua kuwa DHEAS ambayo ni homoni inayo patikana kwenye mwili inaweza badilika iwe testosterone ilipunguka kwa asilimia 22.2 katika kikundi cha resveratrol na kuongezeka kwa asilimia 10.5 katika kikundi cha placebo.

Resveratrol na kisukari

Utafiti huu ulipata kuwa resveratrol inaweza saidia na kisukari. Watafiti pia waliangalia kilicho tendeka kwa insulin kwa wanawake walio chukua resveratrol.

Matokeo yana pendekeza kuwa resveratrol inaweza boresha uwezo wa mwili wa kutengeneza insulin na kupunguza hatari za kupata kisukaro," mwandishi mkuu Antoni Duleba alisema. "Kiongezo hicho cha weza saidia katika kupunguza hatari ya matatizo ya metaboli yaliyo kawaida katika wanawake walio na PCOS.

Soma Pia:Divai Ya Mnazi: Kinywaji Hiki Kina Faida Za Kushangaza

Written by

Risper Nyakio