Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba: Egusi Ni Nzuri Kwa Mimba?

Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba: Egusi Ni Nzuri Kwa Mimba?

Wanawake wenye mimba mara nyingi wanashauriwa kukaa mbali na baadhi ya vyakula. Ila je, egusi ni nzuri kwa mimba? Soma ujue iwapo ni nzuri kuila.

Safari ya mimba ni kipindi ambacho mama anapaswa kuwa makini sana na vitu vingi. Hii ni kwa sababu sio afya yako tu, mbali una kiumbe kingine kinacho kua ndani yako na ni jukumu lako kuhakikisha kuwa afya ya nyote wawili iko salama. Unapaswa kuwa makini na aina ya chakula unacho kila, dawa unazo kunywa na maisha yako. Wanawake wengi hunywa supu nyingi wanapokuwa na mimba kwa sababu ya viungo asili vinavyo tumika kutengeneza supu hizi. Ila, supu ya egusi ni nzuri kwa mimba?

Je, Supu Ya Egusi Ni Nzuri Kwa Mimba?

Is egusi soup good for pregnancy?

Egusi ni aina ya supu iliyo maarufu sana hasa sehemu za Nigeria. Inatokana na mbegu zenye ufuta na protini wa aina fulani za mimea kama vile tikiti, squash na gourd. Ni vigumu kuingia kwa hoteli yoyote na ukose supu ya egusi. Kama jina linavyo sema, egusi ndiyo kiungo kikuu. Viungo vingine ni kama:

  • Maji
  • Mafuta nyekundu
  • Mboga (majani kali, spinachi, ugu)
  • Pilipili
  • Shrimps
  • Samaki
  • Nyama ya Ng'ombe
  • Crayfish
  • Na viungo vingine vya ladha

Is egusi soup good for pregnancy?

Egusi ina faida nyingi za kiafya, na sio tu kwa wanawake wenye mimba, mbali kwa watu wote wanao kula. Vitamini B1 na B2 vinavyo kuwa kwenye egusi vinasaidia kuboresha hamu ya kula unapokuwa na mimba. Egusi ina wingi wa vitamini kama vile Vitamini E na alpha-tocopherol. Vitamini E inafanya kazi kuimarisha afya ya ngozi yako na kusaidia kupunguza kukauka kwa ngozi na matatizo mengine ya ngozi unapokuwa na mimba. Huku alpha-tocopherol ikiwa kwa bidhaa nyingi za utunzi wa ngozi, na kusaidia kupunguza alama za uzee kwenye ngozi.

Cha zaidi ni kuwa baadhi ya wanawake hutaabika na kukosa maji tosha mwilini wanapokuwa na mimba. Ulaji wa egusi utasaidia na matatizo kwa sababu inasaidia kuimarisha uchakataji wa chakula unacho kula. Fibre ya lishe iliyoko kwenye egusi pia inasaidia kudhibiti mwendo kwenye tumbo unapokuwa na mimba.

Je, egusi ni nzuri kwa mama mjamzito? Tazama faida zaidi za supu hii

is egusi soup good for a pregnant woman?

Methanol inayo toka kwenye egusi inatumika kama njia ya kitamaduni ya kupunguza kufura kwa mwili. Wanawake wengi wenye mimba hufura kwenye miguu. Kwa hivyo, ulaji wa egusi utasaidia kupunguza kufura unapokuwa na mimba.

Pia, fatty acids zilizoko kwenye egusi kuna maana kuwa zinaweza kusaidia kupunguza kiwango cha cholesteroli kilichoko mwilini mwako. Cholestrol nyingi ina julikana kusababisha ugonjwa wa moyo. Kuna viungo vingine vinavyo tumika kutayarisha supu ya egusi. Samaki, shrimps na mboga na zote zina afya kwa mama mwenye mimba, hasa mboga. Kwa hivyo, ni kweli kuwa egusi ni nzuri kwa mama mwenye mimba.

Kuna supu zingine zenye afya ambazo unaweza kunywa unapokuwa na mimba. Supu hizi zina ladha na faida kwa afya yako na ujauzito wako. Supu ya mboga ni nzuri kwako na mtoto wako. Mboga zina egemeza ukuaji wa mtoto wako kwa sababu ya vitamini nyingi zilizoko. Wakati ambapo samaki na supu ya pilipili ya mbuzi inasaidia wanawake kuto pata kichefu chefu wanapokuwa na mimba. Pia, supu ya okra iko kwa orodha ya supu mbora za mama mjamzito. Okra ina fibre na ni nzuri kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto wako.

Soma pia: Chakula Cha Mimba: Je, Ni Salama Kwa Mama Mwenye Mimba Kula Kitunguu Saumu

Written by

Risper Nyakio