Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Emilia Philips Nouah

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Emilia Philips Nouah

Huenda watu wengi wakakosa kulifahamu jina hili Emilia Philips Nouah na sababu kuu ni kuwa Ramsey Nouah na bibi yake wanaishi maisha yao mbali na vyumba vya habari. Ni vigumu kupata habari zozote kuhusu familia ya Nouah kwenye mitandao. Familia hii inajivunia kuishi maisha yao ya kawaida mbali na macho ya kila mtu.

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Emilia Philips Nouah

Chanzo: premiumtimesng.com

Ila, kwa kweli, Emilia Philips Nouah ni nani na amewezaje kukaa mbali na mitandao kwa wakati mrefu hivyo?

Ramsey Nouah ni nani?

Kabla tuanze kufumbua Mrs. Nouah ni nani, lazima kwanza tuongee kuhusu bwana yake. Bwana Nouah anajulikana kwenye Nollywood na anapendwa na wengi. Huenda akawa yeye ndiye kipenzi cha wengi kwenye televisheni zetu za sinema za ki Nigeria. Mwigizaji wetu mashuhuri tunaye mpenda zaidi ametoka mbali kutoka kuwa kinyozi na kuwa mwigizaji anaye tatizika na hatimaye kuwa miongoni mwa waigizaji mashuhuri wa wakati wote Nigeria.

Mwigizaji huyu mwenye ngozi nyepesi wa Nigeria na urithi wa kiisraeli. Nouah alikuwa Lagos na kujiunga na Chuo Kikuu cha Lagos, alipopata shahada ya Mass Communications. Alionekana kwa mara ya kwanza kwenye televisheni katika miaka ya 1990 kwenye programu ya televisheni ya Fortunes na kutoka hapo akawapendeza watu wengi wanao penda sinema za Nollywood kutoka sehemu tofauti duniani kote.

Emilia Philips Nouah

source: premiumtimesng.com

Ameigiza katika sinema nyingi na zile maarufu zikiwa kama vile My Love, 30 Days in Atlanta, The Battle of Love, The Figurine, True Love, Silent Night, na Gbomo Gbomo Express.

Tuzo za Ramsey Nouah’s

Mwigizaji huyu ameshinda tuzo nyingi zaidi na za juu zaidi zikiwa tuzo la The Africa Movie Academy na tuzo zingine nyingi za uigizaji.

Je, bibi yake Ramsey Nouah’s, Emilia Philips Nouah ni nani?

Mbadala ilivyo na wachumba wa watu mashuhuri wengine, huenda ukapatana na bibi yake Ramsey Nouah bila kumjua. Hii ni kwa sababu ndoa yao haifiki kwenye kurasa za makala na kurasa za habari za watu mashuhuri. Wakati mwingi, tunamskia wakati ambapo bwana yake anapatiana mahojiano na kumsifu kwa kumpa egemezo kuu.

Emilia Philips Nouah amekuwa katika ndoa na Ramsey Nouah kwa miaka 18. Katika uhujiano wa hivi karibuni, hivi ndivyo bwanake alisema kumhusu: “Bibi yangu anaamini katika kuishikilia ndoa yetu na mambo yote mbali na watu. Kwa hivyo watu wanapo niuliza jinsi tumekuwa pamoja kwa muda mrefu hivi, jibu langu ni: mke wangu ndiye gundi inayo ishikilia nyumba yetu pamoja.” Wanandoa hawa wame barikiwa na watoto watatu.

Soma pia: Good news for women with PCOS who wish to get pregnant

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio