Endometriosis ni nini? Endometriosis ni hali ambapo tishu inayofanana na kuta ya endometrium hukua nje ya mfuko wa uzazi. Tishu inayokua nje ya uterasi huwa tofauti na tishu ya endometrium iliyoko ndani ya uterasi. Ila, tishu hizi mbili zina mambo sawa. Tishu hii huathiriwa kwa njia sawa na homoni za kipindi cha hedhi kama tishu ya endometrium. Tishu hii huvimba na kutoa damu kama tishu ya endometrial, ila hakuna mahali pa kutupa uchafu ule pamoja na damu.
Tishu inayokua nje ya uterasi pia inaweza kukua sehemu zingine za mwili lakini mara nyingi huathiri sehemu ya pelviki, ovari, mirija ya ovari, tishu zinazoegemeza uterasi na sehemu ya nje ya uterasi.
Ishara za endometriosis

- Maumivu makali ya sehemu ya chini ya mgongo
- Maumivu kwenye pelviki
- Uchungu mwingi wakati wa kipindi cha hedhi
- Damu kwenye haja kubwa
- Kutapika
- Kichefuchefu
- Uchovu wa kupindukia
- Kuhisi uchungu wakati wa ngono
- Vipindi vya hedhi vinavyodumu zaidi ya siku 7
- Kutatizika kupata mimba
Athari za endometriosis kwa afya
- Kuongeza nafasi za kutatizika kutunga mimba kwa asilimia 50
- Kuwa na mwako ama inflammation
- Uvimbe kwenye ovari
Vipimo vya endometriosis
Ni vigumu kwa wataalum wa kiafya kudhibitisha kuwepo kwa endometriosis kwani hakuna kipimo maalum chake. Ishara zake huenda zikakaribiana na za magonjwa tofauti. Njia ambazo zinaweza kutumika kufahamu iwapo mwanamke ana hali hii ni kipimo cha biopsy, laparascopy, kipimo cha pelviki na scan ya MRI.
Endometriosis ni nini: Matibabu ya endometriosis

Hakuna tiba ya endometriosis lakini kuna baadhi ya mbinu zinazosaidia kupunguza uchungu na ishara za endometriosis.
Kuna baadhi ya dawa zinazotumika kupunguza uchungu. Kama vile advil, hata hivyo ni muhimu kupatiwa orodha ya dawa bora na daktari.
Huenda daktari akashauri upasuaji kutoa tishu zisizohitajika iwapo mbinu zingine za matibabu hazitafaulu. Katika visa vingine, huenda hysterectomy ikafanyika ambapo uterasi zote mbili zinatolewa.
Huenda daktari akashauri tembe za kudhibiti ujauzito ama mbinu za uzazi wa mpango za homoni. Mabadiliko ya homoni na kupunguka kwa estrogen mwilini kunasaidia kudhibiti ukuaji wa tishu zisizohitajika na kuboresha nafasi za rutuba mwilini.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Kweli Kuhusu Endometriosis: Imani Kuhusu Endometriosis Na Iwapo Ni Kweli Ama La