Chokleti hutoka kwa mmea wa cacao ulio na viwango vingi vya madini na antioxidants. Chokleti iliyochakatwa huwa na sukari, maziwa, siagi ya cocoa na kiwango cha cacao. Tuna angazia manufaa ya kiafya ya chokleti nyeusi.
Chokleti nyeusi ina madini mengi kama vile zinc, magnesium na iron. Pia ina antioxidants zinazofahamika kama flavonoids ambazo zina manufaa ya kiafya.
Manufaa ya kiafya ya chokleti nyeusi

Gramu 100 za chokleti nyeusi huwa na asilimia ifuatayo ya virutubisho:
- Kalori 604g
- Protini 7.87g
- Wanga 46.36g
- Ufuta 43.06g
- Sukari 24.23g
- Zinc 3.34g
- Fiber 11.00g
- Magnesium 230.0g
Chokleti nyeusi ina flavanols, polyphenols na theobromine. Sawa na vyakula vingine vinavyochakatwa, chokleti hupoteza kiwango cha cocoa inapochakatwa. Huku viwango vya polyphenol vikipotezwa katika mchakato, siagi ya cocoa, maziwa na sukari huongezwa. Manufaa ya kiafya ya cocoa ni kama vile:
- Kupunguza cholesteroli hatari mwilini
- Kupunguza mwako
- Kupunguza free radicals
- Kuboresha mzunguko wa damu
- Kupunguza shinikizo la damu
- Kuongeza uwezo wa akili wa kufanya miunganisho kati ya neurons
Antioxidants
Chokleti nyeusi ina compounds nyingi zilizo na antioxidants kama flavanols na polyphenols. Antioxidants zinasaidia kuepuka oxidative stress ambayo huchangia katika maradhi kama ugonjwa wa moyo, kisukari, saratani na ugonjwa wa macho.
Kolesteroli
Chokleti nyeusi ina theobromine na polyphenols zinazosaidia kupunguza viwango vya kolesteroli mbaya mwilini na kuongeza viwango vya kolesteroli nzuri.

Shinikizo la damu
Chokleti nyeusi ina flavanols zinazosisimua utoaji wa nitric oxide mwilini. Nitric oxide inasababisha mishipa ya damu kupanuka na kuboresha mzunguko wa damu mwilini huku shinikizo la damu likipunguka. Manufaa ya chokleti kupunguza shinikizo la damu huwa zaidi kwa watu wazee ikilinganishwa na watu wachanga.
Ugonjwa wa moyo
Chokleti nyeusi ina flavanols zinazoathiri kolesteroli mwilini na shinikizo la damu, ambazo zinahusiana na ugonjwa wa moyo. Kula chokleti nyeusi mara kwa mara kunaweza kupunguza nafasi za mtu kupata ugonjwa wa moyo.
Chokleti nyeusi ni chanzo cha madini na antioxidants na huwa na kiwango kidogo cha sukari ikilinganishwa na maziwa. Kulingana na utafiti, manufaa ya kiafya ya chokleti nyeusi ni kama kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, kupunguza mwako na kuboresha utendaji kazi wa ubongo.
Soma Pia: Umuhimu Wa Lishe Bora Mapema Katika Mimba Ni Upi?