Faida 9 Za Tikiti Kwa Mama Mwenye Mimba

Faida 9 Za Tikiti Kwa Mama Mwenye Mimba

Tikiti ni tunda lenye rangi ya kupendeza ya pinki na linapaswa kuwa rafiki wa karibu zaidi kwa wanawake wenye mimba. Lina saidia kupunguza ugonjwa wa asubuhi na kusaidia watu kuwa na maji tosha mwilini.

Kuwa mama ni mojawapo ya hisia za kupendeza zaidi duniani. Lakini mimba huja na miezi tisa ya kuto starehe kusiko elezeka, ukihusisha hamu ya vyakula, mhemko wa hisia na kusikiza ushauri usio isha. Mojawapo ya vitu utakavyo sikia mara nyingi ni 'kula matunda kwa wingi'. Lakini kuna matunda mengi ambayo hauwezi kula. Kwa bahati nzuri, tikiti sio mojawapo ya matunda hayo. Hakikisha una sahani yako ya tikiti tukiji elimisha zaidi kuhusu faida za tikiti kwa mama mwenye mimba.

Faida za kupendeza za tikiti kwa mama mwenye mimba

benefits of watermelon during pregnancy

Hapa chini kuna manufaa ambayo wanawake wenye mimba hupata wanapo kula tikiti. Lakini kwanza tujifunze zaidi kuhusu tunda hili.

Kujua zaidi kuhusu tikiti maji
  • Jina la kisayansi — Citrullus lanatus
  • Asili — Southern Africa

Kama jina linavyo ashiria, tikiti ni tunda lenye asilimia 92 ya maji. Lina ladha tamu na ya kisharubati na huwa mojawapo ya uchaguzi bora kunapokuwa na joto jingi. Tunda hili lina virutubisho vingi hata Vitamini A, C, B6, magnesium na potassium. Tikiti pia ina fiber nyingi na kuiweka kwenye kikundi cha vyakula vinavyo fanya mtu ahisi kushiba. Mbegu za tunda hili pia zina liwa.

Tuchambue umuhimu wa tunda la tikiti katika ujauzito.

Faida za tikiti unapokuwa mjamzito ni zipi?

pregnant-woman-

Kupunguza kiungulia

Tikiti ni laini kwa tumbo na bomba la chakula. Wanawake wajawazito huwa na matatizo mengi ya kuchakata chakula kama kiungulia na acidity. Lakini tikiti ina uwezo wa kupunguza uchungu na matatizo haya na kukufanya upone. Kwa hivyo ukipata kiungulia tena, kula tikiti kutatua tatizo hilo na utakuwa sawa.

Kupunguza kuvimba miguu na mikono

Oedema ama kufura kwa miguu na mikono ni tatizo la kawaida katika ujauzito. Tikiti ni asilimia yake kubwa ya maji hupunguza kuziba mishipa na misuli yako na kuepusha oedema.

Hupunguza ugonjwa wa asubuhi

Tikiti ikiliwa wakati wa asubuhi, inakusaidia kuhisi vyema na kutuliza tumbo yako na kuanza siku yako vyema. Pia inasaidia na virutubisho na kukupa nishati na kukuepusha na ugonjwa wa asubuhi. Ni wazo njema kwa wanawake wenye mimba kuanza siku zao na glasi ya sharubati freshi ya tikiti. Ijaribu leo!

Kusaidia kuepusha upungufu wa maji mwilini

Ikiwa wewe ni mama mjamzito, ni vyema kunywa maji mengi kuepusha ukosaji wa maji tosha mwilini. Ukosefu wa maji mwilini husababisha kubana kusiko komaa na kusababisha kujifungua kabla ya wakati. Tikiti ina asilimia 90 ya maji na kula tunda hili ni njia nzuri ya kuwa na maji tosha mwilini.

Manufaa zaidi ya tunda hili la tikiti wakati wa ujauzito

faida za tikiti kwa mimba- sharubati ya tikiti

Kupunguza uchungu wa hedhi

Wakati wa ujauzito, mwili wako hupitia mabadiliko mengi. Uzito mwingi na homoni zinaweza fanya misuli na mifupa yako kuuma. Kula tikiti kunasaidia mwili wako kuishi vyema na mabadiliko haya na kutuliza uchungu wa misuli yako.

Kuepusha kukauka ngozi 

Wanawake wengi wenye mimba huwa na shida ya ngozi kukauka. Tatizo hili linalo wasumbua huenda lika ingilia kati kung'ara kwa ujauzito.

Tikiti husaidia kuweka mwendo wa tumbo uwe laini na kurahisisha uchakataji wa chakula. Jambo hili huathiri ngozi. Ili kupunguza tatizo la ngozi kukauka linaweza epushwa kwa kusafisha mwili mara kwa mara. Kwa hivyo kula tikiti yako ikiwa ungependa kuwa na ngozi inayo ng'aa.

Kuboresha mfumo wa kinga

Unapokuwa na mimba, mwili wako unakula chakula cha watu wawili- wewe na mwanao. Tatizo lolote kwenye afya yako lina athiri ukuaji na maendeleo ya afya ya mtoto aliye tumboni mwako. Lakini kula tikiti mara kwa mara kuna weza boresha mfumo wako wa kinga.

Tunda hili lina lycopene, ambayo ni antioxidant inayo ipa rangi nyekundu. Lycopene inasaidia kupunguza nafasi za kupata pre-eclampsia kwa asilimia 50. Pia ina jukumu la kujenga mfumo wa kinga ambayo huenda ikashuka wakati wa ujauzito.

Kupunguza kuvimbiwa

Kuvimbiwa ni tatizo la kawaida ambalo wanawake wenye mimba hukumbana nalo. Tikiti ni njia salama na ya kuaminika ya kutatua matatizo ya tumbo. Lina wingi wa fiber inayo boresha kutengeneza kinya, kiwango chake cha maji kina saidia kutengeneza njia ya kupitia na kutengeneza shinikizo la tumbo.

Kuegemeza ukuaji wa mifupa ya kiinitete

Tikiti ina wingi wa kalisi na potassium; madini yanayo saidia kuboresha ukuaji wa mifupa ya mtoto. Kwa hivyo kumbuka kuliongeza tunda hili kwenye lishe yako unapokuwa na mimba!

Kuwa mwangalifu!

faida za tikiti kwa mimba- sharubati

Hata kama tunda la tikiti lina manufaa mengi kwako na kwa afya ya mtoto wako, lina athari hasi; hasa unapo kula tunda hili zaidi ya inavyo hitajika. Tuangazie:

  • Kula tikiti kwa sana kuna weza sababisha viwango vya juu vya glucose ya damu na kusababisha kisukari cha gestational
  • Ikiwa unatumia tikiti kusafisha mfumo wako, huenda uka toa virutubisho muhimu kwenye mwili wako
  • Tikiti huharibika mbio sana. Kwa hivyo jaribu usile tikiti yoyote ambayo imekuwa imefichuliwa kwa muda mrefu sana kwani huenda ikasababisha kutapika ama kichefu chefu. Kula tikiti zilizo katwa zingali freshi na sharubati iliyo freshi pia
  • Hatimaye, wasiliana na daktari wako ukipanga kuhusisha tikiti kwenye lishe yako. Ata kushauri viwango vinavyo faa ili upate manufaa mengi

Kula tikiti ukiwa na mimba ni salama, lakini kumbuka kula kwa kujidhibiti na usile viwango vingi.

Vyanzo: WebMD, United States Department of Agriculture

Soma pia: Banana Benefits: how bananas can help you before and after your pregnancy

Written by

Risper Nyakio