Kwa miaka mingi, asali imekuwa mojawapo ya bidhaa zinazotumika kama tiba. Inafahamika kuwa na manufaa ya kiafya na kutumika badala ya sukari. Je, kuna faida ya asali mbichi kwa mjamzito?
Faida ya asali mbichi kwa mjamzito

- Kuupa mfumo wa kinga nguvu
Katika ujauzito, mama anahitaji kuwa na mfumo wa nguvu kumkinga dhidi ya kupata maambukizi ya aina yoyote. Ujauzito huwa kipindi nyeti kwa mama na mfumo wake wa kinga huenda ukaathiriwa. Asali ina hozi za antioxidants na antibacterial zinazosaidia kuboresha mfumo wa mama wa kinga na kupigana dhidi ya maambukizi. Ni vyema kwa mama mjamzito kuongeza asali kwenye lishe yake.
2. Kupigana dhidi ya mafua na baridi
Asali ina hozi za kukinga dhidi ya virusi na kuzidisha nguvu. Zinasaidia kulinda dhidi ya kupata mafua. Wanawake wajawazito wanaweza faidika kwa kuongeza asali kwenye vinywaji kama vile chai wanapoinywa.
3. Kuponya kikohozi na koo chungu
Asali inafahamika kama dawa ya koo chungu na kikohozi. Inapochanganywa na ndimu, kitunguu saumu na tangawizi husaidia kuponya kikohozi. Hii ni dawa maarufu na imetumika kwa miaka mingi.
4. Kupunguza uchungu kufuatia vidonda vya tumbo
Kula asali mara kwa mara husaidia na kupunguza uchungu wa vidonda vya tumbo na pia kuponya vidonda hivyo kwa pamoja. Wanaotatizika na hali ya kuwa na asidi zaidi mwilini ama maambukizi ya H.pylori wanaweza kufaidika na asali. Hata hivyo, ikiwa una vidonda vya tumbo, wasiliana na daktari wako akupe kibali cha kutumia asali.

5. Kuzuia dhidi ya mzio
Asali ambayo haijachakatwa huwa na pollen inayofahamika kusaidia kuboresha kinga dhidi ya mizio. Kula asali mara kwa mara husaidia mwili kupata kinga tosha dhidi ya antigens ambazo zinaweza ibuka katika mimba.
6. Kutatua hali ya kukosa usingizi
Kwa watu wanaotatizika kupata usingizi, mojawapo ya njia bora zaidi kupata usingizi kwa urahisi ni kula asali. Ulaji wa asali dakika chache kabla ya kulala unasaidia kupunguza mawazo mengi. Na kwa hivyo kuboresha kiwango cha usingizi. Mjamzito anayetatizika na hali ya kukosa usingizi anaweza ongeza asali kwenye chai kisha anywe kabla ya kulala.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Mimba Ya Rihanna Na Staili Yake Ya Mavazi Katika Mimba