Kwa mimba yoyote isiyo na matatizo, ama mimba yenye afya, tendo la ndo huwa lenye starehe na kufurahisha. Je, unafahamu faida ya kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito?
Tendo la ndoa huwa na manufaa ya kiafya, kiakili, kupunguza mawazo, wasiwasi na kuboresha utangamano kati ya wanandoa. Wanandoa huenda wakawa na shaka kuwa kufanya mapenzi katika mimba kunahatarisha maisha ya mtoto. La, mtoto amezingirwa na amniotic sac inayomlinda.
Hamu ya kufanya mapenzi katika ujauzito

Ili kuwa na wakati wa kusisimua, ni muhimu kuwa na mazungumzo wazi. Hamu ya mama ya kufanya tendo la ndoa katika mimba hubadilika mara kwa mara kufuatia ongezeko la homoni mwilini. Huku wanawake wengine wakipata hamu iliyoongezeka ya kufanya mapenzi, wengine huenda wakakosa hamu ya kufanya mapenzi, kila mwanamke ni tofauti.
Faida ya kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito
1.Kufika kilele kwa kirahisi
Wanawake wengi huripoti kufika kilele kwa kirahisi na nguvu zaidi katika ujauzito na kuwafanya kutosheleka zaidi. Tendo la ndoa limedhihirishwa kupunguza mawazo, linawasaidia wanawake wajawazito kutulia kimawazo. Katika muhula wa pili, ongezeko la homoni na mzunguko wa damu mwilini huchangia pakubwa katika ongezeko la hamu ya kufanya ngono.
2. Zoezi Bora
Mjamzito anapofanya mapenzi, anafanya mazoezi na kupunguza kalori zaidi mwilini. Sawa na mazoezi mengine, tendo la mapenzi linapunguza shinikizo la damu. Shinikizo la damu katika mimba huwa na hatari kubwa. Kufanya mapenzi mama anapokuwa na mimba kunashauriwa. Kunamsaidia kulala vyema usiku baada ya kipindi chao.

3. Kuboresha kinga ya mwili
Mtu anapofanya mapenzi, kemikali zinazotolewa katika kitendo hicho husaidia kuongeza kinga ya mwili. Kemikali ya lgA ni kingamwili inayosaidia kulinda dhidi ya mafua na maambukizi mengine.
4. Furaha iliyoongezeka
Mwanamke anapofika kilele, endorphins hutolewa mwilini zinazomsaidia mama kuhisi furaha na kutulia zaidi.
5. Kujiamini zaidi
Mabadiliko mwilini katika mimba huenda yakamfanya mwanamke kuwa na hisia tofauti kuhusu mwili wake. Huenda akahisi kuwa havutii ama kupendeza kama hapo awali. Hata hivyo, kufanya mapenzi kunamsaidia kujiamini zaidi na kumfanya ahisi kuwa ako mzima.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kufanya Mapenzi Katika Mimba Ni Salama Kwa Mtoto? Maswali Kuhusu Ngono Katika Mimba