Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

Utafiti wa hivi majuzi una onyesha faida za kiafya za kulala mchana na umuhimu wa kulala kwa angalau dakika 30 wakati wa alasiri kila siku.

Wana Kenya ni mojawapo ya watu wasio pata usingizi tosha duniani kote. Hasa wanao ishi mji wa Nairobi. Maisha haya ngoji mja na inawa bidi kupiga blanketi mateke mapema sana ili kuanza shughuli zao za kila siku. Msongamano wa magari usio isha una wafanya watu kukaa muda mrefu kwa magari kabla ya kufika kazini, ama mahali wanapo elekea asubuhi na kufika nyumbani usiku sana. Wikendi ni wakati wa kuburudika na marafiki na wana jamii na wakati mwingine kupiga sherehe usiku wote. Usingizi ni muhimu sana kwa afya nzuri. Suluhu ni kulala mara moja ama mbili kwa siku. Tuna kuelezea kuhusu faida za kiafya za kulala mchana.

Kulingana na utafiti mpya, kulala kwa dakika chache mchana kuna faida kwa afya yako. Watafiti kutoka Greece wa hospitali ya Asklepieion wali watafiti watu 212. Na wakapata kuwa wanao chukua dakika chache mchana wana viwango vidogo vya shinikizo la damu. Kwa ujumla, kulala mchana kuna husishwa na kupunguka kwa 5 mm Hg katika shinikizo la damu. Kuna zaidi!

Faida za kiafya za kulala mchana

faida za kiafya za kulala mchana

  • Kuboresha uwezo wako wa kukumbuka

Utafiti una dhihirisha kuwa usingizi unasaidia pakubwa katika kukumbuka matukio. Kulala kunaweza kusaidia kukumbuka mambo uliyo soma siku ikianza sawa na usingizi wa usiku. Kulala kuna kusaidia kuto sahau mambo kama uwezo wa kukumbuka yaliyo semwa na mengine.

  • Huenda ukaweza kugundua mambo fiche

Kulala hakukusaidii, kukumbuka yaliyo semwa tu. Ila, kutakusaidia ubongo wako kushikanisha mambo na kugundua yaliyo fichwa. Katika somo moja, kulala kuna kusaidia kuelewa mambo uliyo yasikia siku yote.

  • Kuna boresha ubunifu wako

Mojawapo ya faida za kiafya za kulala zitakazo kushangaza ni kuboresha ubunifu wako. Ushawahi kuamka na fikira bunifu? Dakika 70-90 baada ya kulala, sehemu ya ubongo ina amshwa inayo husika na ubunifu na kuota. Usingizi huu unakusaidia kuleta mawazo pamoja na kupata majibu.

faida za kiafya za kulala mchana

  • Kuboresha mhemko wako

Ikiwa unahisi hauna raha, jaribu kulala kwa dakika chache kuinua roho na hisia zako. Kulala ama hata kupumzika kwa lisaa limoja kutakusaidia kuhisi vyema. Wataalum wana sema kupumzika kunako tokana na kulala na kupumzika kunasaidia na mhemko wako, ikiwa utalala ama la.

  • Ungependa kutahadhari na kuwa makini zaidi? Lala

Ukianza kuhisi usingizi baada ya kula chamcha chako, hauko peke yako. Chukua mapumziko ya angalau dakika 20 ulale.

  • Kulala ni bora ikilinganishwa na kafeini

Ikiwa unahisi kuchoka lakini una kazi ama kusoma ili umalize, unaweza faidika zaidi kutokana na usingizi kuliko kafeini ama kahawa. Ikilinganishwa na kafeini, kulala kunaweza leta makumbusho bora na kusoma.

what happens when you oversleep

  • Faida za kiafya za kulala: Kupunguza fikira nyingi

Ikiwa una shinikizo nyingi, kulala kunaweza kusaidia kupunguza fikira nyingi na kuboresha mfumo wako wa afya. Wataalum wana amini kuwa kulala dakika 30 kunaweza kusaidia.

  • Kulala mchana kunaweza kusaidia kulala vyema usiku

Hata kama inaonekana kama haiwezekani, kulala mchana kunaweza saidia watu wazima kulala vyema zaidi usiku. Utafiti umeonyesha kuwa kulala dakika 30 katika ya saa saba na saa tisa mchana pamoja na mazoezi ya wastani; kama vile kutembea na kujinyoosha kuna saidia usingizi wa usiku. Afya ya fizikia na kiakili inaweza boreshwa pia.

Sleep Foundation            WebMD

Soma Pia:Utafiti Unadhibitisha Kuwa Wanawake Wanahitaji Usingizi Zaidi Kuliko Wanaume

Written by

Risper Nyakio