Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi

Tendo La Ndoa Ni Bora Kwa Afya Na Uhusiano Wako: Kwa Njia Hizi

Faida za tendo la ndoa kwa afya yako ni kama vile kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kupunguza shinikizo ya damu mwilini.

Tendo la ndoa ni muhimu sana maishani kwa watu walio funga ndoa. Faida kuu inayo husishwa na ngono katika uhusiano ni watoto. Lakini mbali na uzalishaji, kuonana kingono kuna manufaa mengi kwako na kwa uhusiano wako. Mbali na furaha na kutosheleka, kuna faida za kiafya za tendo la ndoa. Kwa hivyo pia, kuna manufaa ya kiakili, kijamii na hisia. Tume angazia baadhi ya ujumbe jinsi kufanya mapenzi ni vyema kwa akili na afya yako kulingana na sayansi. Hatimaye, kuna baadhi ya mambo ya kiafya ambayo unaweza angazia.

faida za kiafya za tendo la ndoa

Faida za tendo la ndoa kwa afya yako ni nini?

Afya ya kimapenzi inapaswa kuwa na maana zaidi kwako kuliko kuepuka mimba na magonjwa yanayo sambazwa kingono. Ni kuhusu kutambua kuwa ngono ni sehemu muhimu ya maisha yako. Hivi ndivyo unavyo weza kunufaika na maisha ya kingono yenye afya.

  • Kuboresha mfumo wako wa kinga. Katika somo la kinga katika wanandoa, watu wanao fanya mapenzi mara kwa mara wana immunoglobulin A (IgA) kwenye mate yao. Watu wasio fanya mapenzi mara kwa mara (chini ya mara moja kwa wiki) walikuwa na viwango vidogo vya IgA. IgA ni kingamwili inayo kuwa na jukumu la kulinda dhidi ya magonjwa na inasaidia sana dhidi ya HPV (human papillomavirus).
  • Kupunguza shinikizo la damu. Utafiti una shauri kuwa matendo ya kingono yana husika na kupunguza shinikizo la damu, alisema Joseph J. Pinzone, mkurugenzi mkuu wa Amai Wellness. "Kumekuwa na masomo mengi, lakini somo moja kuu lili vumbua kuwa tendo la ndoa linapunguza shinikizo ya damu ya systolic." Hiyo ndiyo nambari ya kwanza kwenye kipimo chako cha damu.

faida za kiafya za tendo la ndoa

  • Kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo. Maisha mazuri ya kingono ni muhimu kwa mtima wako. Tendo la ndoa linaongeza mpigo wa moyo wako na kusawasisha viwango vya estrogen and testosterone mwilini. Wakati ambapo moja wapo ya homoni hizo ziko chini, unaanza kupata matatizo mengi kama vile osteoporosis na ugonjwa wa moyo.
  • Kupunguza uchungu. Kabla ya kufikia dawa za uchungu, jaribu kufika kilele cha ngono kwanza. Katika tendo la ngono, oxytocin inatolewa mwilini na kusababisha endorphins kutolewa. Kwa sababu ya opiates asili, tendo la ndoa linapunguza uchungu.
  • Kupunguza mawazo mengi. Kuwa karibu na mchumba wako kunaweza saidia kupunguza mawazo mengi na wasiwasi. Pia, kushikana na kukumbatiana kunaweza achilia homoni ya mwilini ya kuhisi vyema. Utahisi vyema na kupata ujasiri pia.

Kumbukumbu: Web MD

Soma Pia:Faida Za Kiafya Za Tendo La Ndoa Kwa Wanandoa

Written by

Risper Nyakio