Tazama Faida Hizi Za Kiafya Za Manjano (Turmeric)

Tazama Faida Hizi Za Kiafya Za Manjano (Turmeric)

Manjano yana sawazisha shinikizo la damu na kukuepusha kutokana na hypertension. Pia, yanasaidia kupunguza sukari ya damu kwa wanao teseka kutokana na kisukari.

Manjano ni kiungo kinacho tumika katika mapishi kuongeza chakula ladha. Pia kina fahamika kama hawaji. Mzizi wa mmea wa turmeric ndio unao onekana sana kwenye soko na maduka, hata kama bado kuna poda yake baada ya kukaushwa na kusiagwa. Turmeric ni kiungo kikuu katika rojo. Rangi yake ya manjano ina maana kuwa kuna watu wanao itumia kubadilisha rangi ya nywele zao. Manjano yana kiungo chenye nguvu kinacho fahamika kama curcumin na ina changia katika faida za kiafya za turmeric.

Faida za kiafya za turmeric

faida za kiafya za turmeric

Kiungo cha manjano kina manufaa mengi ya kiafya. Profesa Manohar Garg ambaye ni mkurugenzi wa programu ya utafiti ya nutraceuticals katika Chuo Kikuu cha Newcastle ana amini katika hozi zenye nguvu za kiungo hiki. Hapa chini kuna orodha ya manufaa ya kiafya unayo pata unapo tumia kiungo hiki cha hawaji.

1. Inasaidia kupunguza uchungu kwenye viungo

Hii ni mojawapo ya manufaa ya turmeric. Uchungu kwenye viungo huku dhibiti kutembea kutoka mahali pamoja hadi pengine. Ama aina hiyo nyingine inayo fanya viungo vyako vifure ama kukosa kutembea. Uchungu wa viungo huathiri jinsi unavyo tenda kazi zako za kila siku na jinsi unavyo ishi maisha yako, na kusababisha uchungu na kuto starehe. Na uharibifu huu unaweza kuwa wa kudumu usipo utibu bila kukawia. Lakini manjano yanaweza kusaidia na uchungu wako wa viungo.

2. Inasaidia na kukata uzani

Uzito mwingi unaweza sababisha aina zote za matatizo ya kiafya, hata kiharusi, maradhi ya moyo na shinikizo la juu la damu. Kupunguza uzito wa mwili kunaweza kuwa rahisi ikiwa una afya. Lakini ikiwa mwili wako una matatizo kutumia chakula unacho kula vizuri, kupunguza uzito wa mwili kunaweza kuwa tatizo kubwa. Hapa ndipo turmeric ina kusaidia kwa sana. Ina usaidia mwili wako katika njia unao tumia chakula na kulenga ufuta kwenye mwili.

3. Inafanya ngozi yako iwe bora

Wengi wetu tuna taka ngozi yenye afya. Aina ya ngozi ambayo ni laini, yenye afya na isiyo na upele. Ngozi yako ni mojawapo ya viungo muhimu zaidi mwilini mwako. Ina saidia kulinda mwili wako na kusawazisha joto yako. Utaratibu mwingi wa kinyumbani wa kutengeneza uso unatumia hawaji kwa sababu inaweza fanya ngozi yako iwe nzuri zaidi na ing'ae. Inafanya hivi kwa kurekebisha tishu mbio.

4. Inasaidia kupigana dhidi ya maradhi

faida za kiafya za turmeric

Hii ni faida muhimu ya manjano. Maradhi mengi yanaweza athiri utendaji kazi wa mwili. Maradhi kama saratani, kisukari, hyptertension ama maradhi ya kawaida. Na yanaweza sababisha kifo ama kufanya afya ya mwili kudidimia. Lakini manjano yana sawazisha shinikizo la damu na kukuepusha kutokana na hypertension. Pia, yanasaidia kupunguza sukari ya damu kwa wanao teseka kutokana na kisukari. Lakini hayo sio yote. Manjano yana lenga seli za saratani na kusaidia kupunguza uchungu kwa wagonjwa wa saratani.

5. Kuboresha utendaji kazi wa ubongo

Ubongo una dhibiti shughuli nyingi mwilini, za kiakili na kifizikia. Na kula manjano kuta boresha afya yako ya kijumla ya akili. Manjano yana fanya hivi kwa kuboresha jinsi ubongo wako unavyo tuma ishara kwenye sehemu zingine za ubongo na mwili wote. Pia, manjano yana punguza mawazo mengi ya kiakili kwa watu wanao kabiliana na kuto kuwa sawa kiakili, wasiwasi nyingi ama kufilisika kimawazo.

6. Ina boresha mizio

Kwa ujumla, kuna watu ambao hawawezi fanya vitu vingine wakati ambapo watu wengine wata weza kuvifanya kwa urahisi. Kuna madawa ambayo hawawezi chukua, vyakula ambavyo hawawezi kula na vinywaji pia. Pia, wengine wana pata ikiwa vigumu kuishi kwa hali fulani za anga. Mzio unafanyika pale ambapo mwili wako una athariwa na hali fulani. Kama vile kujikuna, kuchemua na kubadilika kwa ngozi. Manjano yana saidia kupigana dhidi ya mizio kwenye mwili.

7. Inasaidia na maumivu ya kichwa

Kuumwa na kichwa huja na aina ya nguvu ambazo zita athiri siku yako yote. Kuumwa na kichwa kunaweza dumu kwa masaa machache ama siku kadhaa. Uchungu huu haupungui kwa urahisi.

Una sababishwa na fikira nyingi, kuketi vibaya, uchovu na kuto lala vya kutosha. Lakini antioxidants zilizoko kwenye manjano zinasaidia kupunguza uchungu huu.

8. Kuboresha mhemko na kupunguza mawazo

Kuna kemikali kwenye ubongo wako zinazo julikana kama 'kemikali za furaha' na homoni za stress. Zote zina husika na mhemko wako na unavyo kumbana na fikira nyingi. Kwa hivyo manjano yana boresha homoni hizi ili uweze kukabiliana na mawazo yote ambayo unaweza kukumbana nayo unapo fanya shughuli zako.

Hakikisha kuwa una ongeza manjano kwenye chakula chako ili ufaidike kutokana na faida nyingi za kiafya zinazo tokana na manjano.

Chanzo: Medical News Today

Soma Pia:Kulala Sana Kuna Athari Hasi Kwa Afya Yako

Written by

Risper Nyakio