Faida 4 Za Kifizikia Unazo Pata Baada Ya Kuwa Baba

Faida 4 Za Kifizikia Unazo Pata Baada Ya Kuwa Baba

Tuna elewa vyema kuwa, kuitwa baba (sawa na kuitwa mama) kuna misuko suko na mema yake, dakika za furaha na kukwazwa kimawazo. Ni ukweli wa ulezi kuwa kulea kiumbe kidogo ni kazi ngumu- kwa wote mama na baba. Tunafahamu kuwa mawazo mengi yanaweza athiri afya yako. Kwa hivyo, kuwa baba kuna athari mbaya kwa afya yako? Ukweli ni kuwa, haina athari mbaya. Kuna faida nzuri za kifizikia za kuitwa baba ambazo huenda haukufahamu.

Faida za kifizikia za kuitwa baba

faida za kifizikia za kuitwa baba, baba

Kulingana na Marcus Goldman, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa The Joy of Fatherhood: The First Twelve Months, "kuitwa baba huja na manufaa mengi ya kiafya. Haiwahimizi wanaume kujitunza zaidi tu mbali huwa na hisia za kuwa na kusudi maishani"

Hivi ndivyo unavyo kuwa na afya zaidi na kupendeza kifizikia kwa kuitwa baba tu.

1.Kuwa na nguvu na kupendeza

Tofauti na imani ya watu wengi, baba hupata himizo kujitunza zaidi kuliko wanaume wengine ambao sio wazazi. Haijalishi ama unamsukuma mtoto wako kwa stroller ama kumrusha angani akitabasamu kwa furaha, mwili wako unafanya mazoezi. Na jambo la kufurahisha zaidi ni kuwa utafurahia unapo fanya hivi.

Lakini ni zaidi ya haya. Wanaume wanapokuwa wazazi, wana hisi wanapata himizo zaidi la kutunza afya yao ya kifizikia ili wawe hapo- wakiwa na nguvu na afya-kutunza watoto wao. Kulingana na daktari Kenneth, "Wanaume wana gundua kuwa wana hitaji kujitunza ikiwa wanataka kuwa karibu na watoto wao."

2. Afya bora ya kingono

Ni wazi kuwa, kufanya mapenzi kuna manufaa bora kwa afya. Masomo imedhibitisha kuwa kutoa manii mwilini kunaweza epuka kupata saratani ya prostrate, kunaweza saidia kuweka kibofu chako na afya, na kukufanya uhisi furaha.

Na je, baada ya kupata watoto, wakati ambapo watu wengi wanaelewa kuwa kufanya mapenzi hudidimia sana?

Ukweli ni kuwa, baada ya kupata mtoto, hisia za kufanya mapenzi huzidi. Kulingana na utafiti, asilimia 94 ya wazazi waliripoti maisha ya kingono yaliyo imarika baada ya mimba. Na wanaume pia walisema kuwa walipendelea miili ya bibi zao baada ya mtoto! Kuwa makini na ubora wa ngono ikilinganishwa na mara mnazo fanya mapenzi.

3. Kupunguza mawazo mengi

faida za kifizikia za kuitwa baba

Wazazi wengi wa kiume wana kiri kuwa mojawapo ya manufaa makubwa zaidi ya kuwa baba ni kuhisi kuwa wana amani zaidi. Kulingana na National Institute of Mental Health, baba wanao husika zaidi katika maisha ya watoto wao hushuhudia ishara chache za mawazo mengi.

Daktari Rosalind Barnett ambaye ni mwanasaikolojia ambaye umakini wake ni mawazo mengi ya maisha ya kikazi kwenye wanaume, alisema. "Wazazi wa kiume wana nafasi chache za kuugua uchungu wa kifua, kukosa usingizi, uchovu, kushindwa kuchakata chakula na kuhisi kizungu zungu." Na kwa sababu afya ya akili na fizikia huwa zime ingiliana, kupunguza mawazo mengi kuna maanisha afya bora ya kifizikia.

4. Kutupilia mbali mazoea mabaya na kuanza mazuri

Kwa sababu baba ana jukumu la afya ya kifizikia ya mtoto, anachukua hatua kuhakikisha kuwa mtoto wake ako salama. Na mojawapo ya hizi ni kutupilia mbali tabia zake mbaya- kama kuvuta sigara- ili afya yake na ya mtoto wako ziwe salama.

Na sio kuvuta sigara tu. Wazazi wa kiume huwa na shinikizo la kutupilia mbali tabia hasi kama kulewa sana ambako hufaidi afya ya kifizikia sana.

Manufaa ya kuwa baba ni mengi. Mumeo ata gundua mambo mapya maishani mwake shukrani kwa mtoto. Na atagundua kuwa ana hisi ana afya na nguvu zaidi kuliko hapo awali! Na kumfanya kuwa na furaha zaidi!

Vyanzo: The Telegraph, Very Well Family

Soma Pia:Vidokezo Vya Kuwa Mama Mwema Kwa Watoto Wako: Sifa 5 Za Mama Mwema

Written by

Risper Nyakio