Faida Za Kitunguu Saumu Kwa Wanaume: Kwa Nini Unapaswa Kuila

Faida Za Kitunguu Saumu Kwa Wanaume: Kwa Nini Unapaswa Kuila

Huenda ukawa hukujua hili ila, kuna faida nyingi za kitunguu saumu kwa wanaume!

Watu wanapofikiria kuhusu kitunguu saumu, mara nyingi wanafikiria kuhusu kiungo kidogo ambacho unaweza ongeza kwa chakula chochote. Lakini kupunguza haya yote, hizi ndizo sababu kwa nini wananume wanapaswa kuongeza kitunguu saumu kwa lishe zao.

Faida za kitunguu saumu kwa wanaume:

Kitunguu saumu ni kiungo kizuri cha kupika

Umejaribu kuweka kitunguu saumu kwenye nyama unapo ipika? Mtu yeyote aliyefanya hivi anaweza kueleza kuwa chakula wakati wote huwa na ladha ya kupendeza. Faida ya kwanza kwa wanaume ni kuwa inaongeza ladha ya chakula chako. Chakula kinapo kuwa na ladha, bila shaka mtu atakula kiwango zaidi na kufaidika kutokana na athari zake chanya.

Kina ponya homa

Kulingana na utafiti ulio chapishwa kwenye Cochrane, kitunguu saumu kimedhibitika kuwa na uwezo dhidi ya viini na vimelea na kukifanya kiwe bora katika kuponya homa. Utafiti huu ulipata kuwa watu wanao kula kitunguu saumu kila siku kwa miezi mitatu huugua homa mara chache ikilinganishwa na watu wasicho kila.

Huku kuna maana kuwa kitunguu saumu kina weza boresha mfumo wako wa kinga uki kiongeza kwenye lishe yako.

Kitunguu saumu kina saidia kupunguza uzito wa mwili

Hakuna njia fupi za kimiujiza za kupunguza uzito wa mwili, ila kitunguu saumu kinaweza egemeza lengo hili kwa wanaume ambao wangependa kupunguza uzito. Lazima upunguze wanga na ufanye mazoezi mara kwa mara ili kilo zako zipungue. Walakini, somo lililochapishwa katika jarida la Journal of Nutrition mwezi wa Novemba 2011 lilipata kuwa kitunguu saumu kikichanganyishwa na lishe ya kupunguza uzito zilisaidia katika kukata uzito wa mwili.

Inaweza punguza shinikizo la damu

Hii ni mojawapo ya faida bora zaidi kwa wanaume kama kitu cha kupunguza shinikizo la damu. Kulingana na utafiti uliofanywa na Daktari Karin Reid na wenzake kutoka chuo kikuu cha Adelaide, ulaji wa kitunguu saumu huenda ukasababisha kupunguza shinikizo la damu kwa watu walio na tatizo la shinikizo la juu la damu.

Kitunguu saumu hupunguza shinikizo la damu ambayo huenda ikasababisha matatizo mengine kama kufa mapema. Katika somo tulilo taja, kitunguu sauamu hufanya kazi vyema na madawa ya matibabu ya shinikizo la damu.

garlic benefits for men

Picha Shukrani kwa: Kjokkenutstyr.net

Inaweza saidia dhidi ya ugonjwa wa Alzheimer na dementia

Una shaka kuwa huenda ukakosa kuwafahamu watoto wako unapo zeeka? Unaweza pumzika, kwa kujua kuwa kitunguu saumu hufanya kazi ya kupunguza athari za uzee kwenye akili yako. Somo lililo fanywa na Carmia Borek na kuchapishwa kwenye jarida la Journal of Nutrition, Volume 136 mwezi wa tatu 2006 lilidhibitisha kuwa kitunguu saumu kina athari ya kulinda ubongo.

Kiungo hiki kina weza punguza athari za dementia na hata vascular dementia. Kina weza linda dhidi ya kuzeeka kwa ubongo, kuimarisha uwezo wa kuelewa na kukumbuka mambo. Mojawapo ya faida za kitunguu saumu kwa wanaume ni kuwa kinaweza ongeza maisha yake.

Kitunguu saumu kinatoa chuma nzito mwilini

Chuma nzito zinaweza kuwa na suumu kwenye mwili. Kuwa na chumu hizi kwa muda mrefu kuna athiri maini, mafua, meno, ngozi, mifupa na sehemu yoyote ile ya mwili.

Kitunguu saumu kina linda viungo vya mwili kutokana na uharibifu wa vyuma hivi kwenye mwili wako. Kwa bahati nzuri, baadhi ya vyakula vinaweza imarisha uwezo wa mwili wa kuchakata vyuma hivi na kuvitoa nje ya mwili na kitunguu saumu ni mojawapo ya vyakula hivi. Faida za kitunguu saumu kwa wanaume zina husisha uwezo wa mwili wa kutoa vyuma hivi na kuboresha ubora wa maisha ya mwanamme.

Kitunguu saumu kina linda viungo vya mwili kutokana na hatari inayo sababishwa na kuwa na vyuma vingi mwilini. Saumu freshi ambayo haijapikwa ina uwezo wa kimatibabu wa kukusaidia kupitisha baadhi ya vyuma hivi kwenye kinyesi ama mkojo.

Ina pigana dhidi ya saratani

Kama tulivyo taja hapo awali, saumu ina uwezo wa kulinda kwa sababu inaweza kupigana dhidi ya bakteria. Huku kunaweza boresha utengenezaji wa DNA na kusimamisha uenezaji na usambaaji wa vitu vinavyo sababisha saratani ama utengenezaji wake. Faida za saumu kwa wanaume zinahusisha kuepusha saratani na kudhibiti saratani.

Ina punguza mzio mwilini

Kula saumu freshi ama vitu vilivyo na saumu ni muhimu katika kuimarisha mfumo wako wa kinga na kunasaidia mwili kulinda dhidi ya homa na mizio mingine. Mwili unapo patwa na mizio, hutoa histamines ambazo huenda zika sababisha kuumwa na kichwa, kukohoa, kujikuna, kuchemua na kadhalika. Saumu husaidia kuziba utoaji wa histamine unapokuwa na mzio.

Faida za saumu kwa wanaume walio na mzio huhusisha kupunguza athari zozote za mzio.

Uwezo dhidi ya kuzeeka mbio

Sote tungependa kubaki wachang. Kitunguu saumu ni dawa bora dhidi ya kuzeeka mbio. Kitunguu saumu kina ongeza ukuaji na maisha ya seli za ngozi, na kukufanya ukae mchanga. Kiwango kinachofaa cha kitunguu saumu kwenye mfumo wako kitamfanya kila mtu ashangae unacho tumia kubaki mchanga.

Kuna faida nyingi za kitunguu saumu kwa wanaume, na ndiyo sababu kwa nini unapaswa kuiongeza kwenye lishe yako. Unaweza ila ikiwa kwa poda iwapo hupendi ikiwa freshi. Kuna uwezekano wa kuishi maisha yenye afya kwa kufanya mabadiliko kwenye mtindo wako wa maisha na kuhakikisha kuwa lishe yako ina wingi wa saumu.

Kumbukumbu: Cochrane; Livestrong; NHS;

The Journal of Nutrition

Healthline

Soma pia: Utafiti: Faida Za Manii Kwa Mtoto Wako Unapokuwa Na Mimba

Written by

Risper Nyakio