Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?

Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?

Mtoto anaye pata maziwa ya mama anakua kwa kasi na kwa njia inayo faa na ni mzima wa afya. Pia uzito wake wa mwili unazidi kuongezeka.

Kunyonyesha mtoto kuna manufaa mengi kwa mama na mtoto wake mchanga. Je, unafahamu faida za kunyonyesha kwa mama? Soma zaidi upate kufahamu.

Faida Za kunyonyesha

  1. Kupunguza hatari ya kuugua

Mama anapo nyo nyesha, anapunguza hatari ya kuugua maradhi ya mifupa kutokuwa na nguvu. Pia kunamlinda dhidi ya magonjwa ya mfumo wa uzazi na saratani ya matiti.

kuumwa na chuchu

2. Kupunguza uzito

Mojawapo ya njia rahisi na za kasi kwa mama aliye jifungua kupunguza uzani wa mwili  ni kwa kumnyonyesha mtoto wake. Mama anashauriwa kumnyonyesha mtoto kila anapo hisi njaa, kwa kufanya hizi, kunachangia katika kupunguza ufuta ulio mwilini mwake.

3. Kuboresha utangamano wa mama na mtoto

Kulingana na sayansi, kitendo cha mama kumnyonyesha mwanawe kina saidia kuboresha utangamano wa wawili hawa. Hii ndiyo maana kwa nini wanawake wana himizwa kuwa nyonyesha watoto wao punde tu baada ya kujifungua.

4. Kulinda dhidi ya kutoa damu nyingi baada ya kujifungua

Homoni mwilini mwa mwanamke hubadilika sana baada ya kujifungua. Mabadiliko haya yana usaidia mwili kurudi ulivyo kuwa hapo awali kabla ya mama kupata mimba na pia kusaidia damu inayo toka kupunguka na kisha kuisha.

Mama anapo nyonyesha mtoto, michakato hii inatendeka kwa kasi na mwili kuanza kurejelea ulivyo kuwa hapo awali baada ya muda mfupi.

faida za kunyonyesha

Manufaa zaidi ya kunyonyesha

Kunyonyesha hakumsaidii mama tu, mbali pia mtoto anaye zidi kukua. Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto. Mbali na kuhisi kuwa ako karibu na mamake, yana faida nyingi za kiafya.

Hiki ndicho chakula cha kipekee ambacho mtoto anaweza kula hadi afikishe umri wa miezi sita. Maziwa ya mama yame jazwa na virutubisho muhimu vinavyo msaidia kukabiliana na kumlinda dhidi ya magonjwa. Pia ana pata virutubisho vyote anavyo hitaji katika ukuaji wake.

Mtoto anaye pata maziwa ya mama anakua kwa kasi na kwa njia inayo faa na ni mzima wa afya. Pia uzito wake wa mwili unazidi kuongezeka kadri anavyo zidi kunyonya zaidi.

Soma PiaOrodha Ya Vyakula Bora Zaidi Kwa Mama Anaye Nyonyesha

Written by

Risper Nyakio