Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

3 min read
Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa MamaFaida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

Tunacho jaribu kusema ni kuwa kunyonyesha kuna manufaa mengi kwako. Na ukiendelea kunyonyesha zaidi ya miezi 24 inayo shauriwa, itakuwa na manufaa kwako na kwa mtoto sana.

Kuna faida nyingi za kisaikolojia za kunyonyesha kwa mama. Utoaji wa maziwa una dhibitiwa na homoni. Kichocheo muhimu zaidi ni prolactin inayo tolewa na pituitary gland kama itiko kwa njaa ya mtoto.

Faida Za Kunyonyesha Kwa Mama

faida za kunyonyesha kwa mama

Prolactin ina jukumu la ukuaji wa mfumo wa lactation katika ujauzito na utoaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha.

Walakini, hii sio jukumu pekee ya prolactin. Ina jukumu nyingine akilini- kukufanya uhisi furaha.

Inafanya hivi kwa kupunguza athari za kichocheo cha fikira nyingi akilini. Prolactin inawasaidia wamama wanao tarajia kwa kupunguza fikira nyingi za ujauzito na kujifungua.

Walakini, mara tu kunyonyesha kunapo koma, viwango vya prolactin hurudi viwango vya kawaida. Kwa hivyo mama anaye nyonyesha anaonekana kuwa mtulivu zaidi kuliko wamama walio tafuta njia mbadala.

Ujauzito, kujifungua, na utunzi wa mtoto- zote zina kwaza. Kunyonyesha kunawasaidia wamama kukabiliana nazo inavyo faa na usaidizi wa kila homoni inayo husika katika utoaji wake wa maziwa. Mwili wa mwanadamu unapendeza kwa kweli!

Kunyonyesha na kutengeneza uhusiano

usingizi wa mtoto

Karibu asilimia 20 ya wanawake hutatizika na kufilisika kimawazo baada ya kujifungua. Ikiwa mama anatangamana vyema na mtoto mapema maishani, uwezekano wa kupata mawazo mengi baada ya kujifungua unapunguka.

Huku kuna imarisha ubora wa utunzi wa mtoto anao mpa mtoto. Kunyonyesha kunamsaidia mtoto kukuza utangamano vyema zaidi. Kwa mama anaye nyonyesa, hata kusikia ama kumwona mtoto baada ya muda mrefu kunaweza fanya aanze kutoa maziwa. Hii ndiyo sababu kwa nini wamama wanao kamua maziwa wakiwa kazini hutazama video ya mtoto wao ama hata kuwa pigia simu waonane.

Utangamano huu huenda zaidi ya hatua za mwanzo mwanzo za kunyonyesha. Utangamano huzidi kuongezeka mtoto anavyo zidi kukua. Hata kama mtoto ameanzishwa chakula, bado anataka maziwa ya mama kwa sababu yanamfanya ahisi vyema zaidi.

Kunyonyesha kunaweza kuwa kazi ngumu

Tunaelewa kuwa kunyonyesha wakati wote hakuji kiasili kwa mama na mtoto. Kwa hivyo huenda kukakwaza. Kuna wakati ambapo mtoto anapolia hata baada ya kunyonyeshwa. Unaweza kuwa na shaka kuwa mtoto hapati maziwa tosha, ama ukahisi kuwa haumtoshelezi.

Baadhi ya wakati, mtoto huuma, na kujeruhi chuchu na kufanya kunyonyesha kuwe kuchungu. Kunyonyesha mtoto kila wakati kunaweza athiri lishe ya mama na kuwa na athari hasi kwa usingizi wake. Maisha yake ya kila siku yana athiriwa pia.

Haya yote yanaweza mfanya mama akome kuendelea kunyonyesha. Lakini wengine huendelea na kukosa kuathiriwa na haya. Ukifanya uamuzi wa kukosa kumnyonyesha mtoto wako, hakukufanyi kutokuwa mama kamili.

Tunacho jaribu kusema ni kuwa kunyonyesha kuna manufaa mengi kwako. Na ukiendelea kunyonyesha zaidi ya miezi 24 inayo shauriwa, itakuwa na manufaa kwako na kwa mtoto sana. Ukipata kuwa unatatizika kunyonyesha, hakikisha kuwa unaongea na daktari wako wa kunyonyesha  ama mama aliye na mtoto mkubwa akudokezee jinsi ya kukabiliana na suala hili.

Vyanzo: Breastfeeding - deciding time to stop. 47 incredible uses of breastmilk

Soma Pia: Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Becoming a Mama
  • /
  • Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama
Share:
  • Changamoto Mama Anazo Kumbana Nazo Anapo Nyonyesha

    Changamoto Mama Anazo Kumbana Nazo Anapo Nyonyesha

  • Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?

    Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?

  • Siri 5 Kuu Za Kuongeza Maziwa Ya Mama Kwa Mama Anaye Nyonyesha

    Siri 5 Kuu Za Kuongeza Maziwa Ya Mama Kwa Mama Anaye Nyonyesha

  • Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

    Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

  • Changamoto Mama Anazo Kumbana Nazo Anapo Nyonyesha

    Changamoto Mama Anazo Kumbana Nazo Anapo Nyonyesha

  • Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?

    Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?

  • Siri 5 Kuu Za Kuongeza Maziwa Ya Mama Kwa Mama Anaye Nyonyesha

    Siri 5 Kuu Za Kuongeza Maziwa Ya Mama Kwa Mama Anaye Nyonyesha

  • Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

    Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it