Malezi bora ni muhimu katika kukuza utu katika watoto. Malezi huwa na panda shuka nyingi, haijalishi iwapo ni mama ama baba anayemtunza mtoto. Watoto wadogo huwa na mahitaji mengi, kando na kifedha, kihisia na wakati. Ni vigumu kwa mzazi kufanya kazi siku nzima anapomlea mtoto katika wiki za kwanza chache. Hata hivyo, wazazi hupata faida kutokana malezi. Tazama faida za malezi kwa baba.
Faida za malezi kwa baba
- Watoto ni motisha ya kuwa na afya

Sote tungependa kulea watoto wetu wawe wenye furaha na afya bora. Mara nyingi, ni azimio la kila baba kuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wake. Hiyo ni motisha tosha ya kumhimiza baba kula na kufanya mazoezi mara kwa mara. Ikiwa unataka watoto wako wakule lishe bora, utajipata ukikula chakula chenye afya na kucheza nawao mara zaidi.
2. Watoto wanahitaji mwendo zaidi
Watoto wadogo wana nishati nyingi na wanapenda kucheza na kukimbia. Ikiwa kabla ya kupata watoto maisha yako yalihusisha kuketi kwa muda mrefu bila kufanya chochote, mambo yatabadilika. Watoto wana mazoea ya kuruka kila mahali, kutoka upande mmoja hadi mwingine na kuenda wasikopaswa. Baba anajukumu la kumfuata kila mahali na kuhakikisha kuwa haendi asikopaswa.
Hata kama linaonekana jambo ndogo, baba atatumia nishati nyingi kumkimbiza kila mahali.
3. Watoto huwapatia baba zao kusudi
Mwanamme anapoitwa baba hupata kusudi zaidi maishani. Na kumfanya atie juhudi zaidi kazini zake ili aweze kukimu mahitaji ya familia yake mpya. Baadhi ya wanaume huenda wakaanzia kazi na biashara zaidi ili wahakikishe kuwa watoto wao hawakosi chochote. Na kuangazia njia zaidi za jinsi ya kutunza familia.
4. Kupunguza kusombwa na mawazo

Watoto huwa kazi nyingi kulea, kila mzazi anaelewa hilo. Hata hivyo, watoto husaidia pakubwa kupunguza mawazo mengi katika watu wakubwa. Kila mzazi anapofika nyumbani na kukaribishwa na mtoto anayemkimbilia na kumuita baba, humjaza na mapenzi na kuhisi kuwa ako sawa. Kulingana na utafiti, baba walio na uhusiano mwema na watoto wao wana nafasi chache za kuugua matatizo ya kiafya kama kukosa usingizi ama uchovu wa kupindukia.
Soma Pia: Kufanya Kazi Hizi Na Watoto Kunawasaidia Kuwajibika!