Faida Fiche Za Manii Mama Anapokuwa Na Mimba

Faida Fiche Za Manii Mama Anapokuwa Na Mimba

Utafiti unadhibitisha kuwa kufanya mapenzi ukiwa na mimba ni muhimu katika kupunguza kichefu chefu. Tuna angazia faida zinginge za manii kwa mimba.

Mengi yamesemwa kuhusu wanawake wenye mimba kufanya matendo ya kindoa na wachumba wao. Huku wengi wakiamini kuwa wanawake walio na mimba hawapaswi kufanya mapenzi na waume wao, kulingana na tamaduni, wengine wana amini kuwa ni sawa kwa mama anaye tarajia kujifungua kufanya matendo ya kingono na waume zao. Wataalum wana yapi ya kusema kuhusu faida za manii kwa mimba?

faida za manii kwa mimba

Faida za manii kwa mama mwenye mimba.

Huenda ikawa kuwa umesikia wanawake na madaktari wakidokeza kuhusu faida za mama mwenye mimba kufanya mapenzi. Inasemekana kuwa kufanya kitendo cha ndoa unapo tarajia husaidia kuboresha usingizi wako usiku, kupunguza shinikizo la damu, na kuwa na mtangamano wa karibu zaidi na mchumba wako.

Wataalum wana shauri kuwa manii yana saidia na:

  • Kutibu ugonjwa wa asubuhi

Kulingana na wataalum, kupata manii mwilini mwa mama aliye na mimba kunamsaidia kuponya ugonjwa wa asubuhi. Mwana saikolojia Gallup alidokeza kuwa mwili wa mama aliye na mimba hujaribu kukataa ama kutoa seli za baba kwenye fetusi kwani ni vitu vipya kupitia kwa kutapika na kuchefu chefu. Alidokeza kuwa tiba ya hali hii ni kuzoesha mwili wako manii haya kupitia kwa kufanya mapenzi ama kuyameza. Utafiti zaidi unahitaji kudhibitisha habari hizi kutoka kwa mwana saikolojia Gallup.

faida za manii kwa mimba

  • Kuepuka preeclampsia

Hii ni mimba yenye hatari kuu, kiwango cha juu cha shinikizo la damu na protini kwenye mkojo. Ina tendeka katika asilimia 5 ama 8 ya mimba yote kulingana na Shirika la Preeclampsia. Hali hii ina hatari nyingi kwani imehusishwa na matatizo kama kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo, kutoboka kwa placenta, kujifungua kabla ya miezi tisa kufika, na matatizo ya figo. Katika kesi ambazo hali hii imezidi, huenda ikasababisha kifo cha mama ama mtoto. Utafiti uliofanyika mmwaka wa 2017 uli shirikisha manii na hali hii ya afya. Kulingana na utafiti huu, wanawake waliofanya mapenzi na wachumba wao walikuwa katika hatari ya kiwango kidogo ya kupata maradhi haya ikilinganishwa na wanawake walio kuwa na zaidi ya miezi sita kabla ya kutofanya mapenzi na wachumba wao.

Manii yana protini ya HLA-G inayo boresha mfumo wa kinga wa mama. Kufanya mapenzi kunasaidia mama kuwa na kinga zaidi manii yanapo achwa mwilini mwake na kumlinda dhidi ya preeclampsia.

Soma pia: Dalili Za Mwanamke Mwenye Mimba Ya Mapacha

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio