Umuhimu Wa Kuishi Na Wanyama Wa Nyumbani

Umuhimu Wa Kuishi Na Wanyama Wa Nyumbani

Zaidi ya nusu yetu husema kuwa walio na mbwa huwa wakarimu kuliko kiwango cha wastani. Asilimia 46 wana amini kuwa kuwatembeza mbya ni mojawapo ya njia za kupata marafiki wapya.

Siku mbaya wakati wote huwa nzuri unapo salimiwa na mbwa anaye punga mkia wake na kukupa mapenzi tele. Kuwa na rafiki mwenye miguu minne kunaweza kufanyia maajabu inapofika kwa afya yako ya kiakili, kifizikia na kijamii. Wanaweza kusaidia kulala vyema, kupunguza uzani na kupata marafiki wapya. Hizi ndizo faida za kiafya za kuwa na mnyama wa nyumbani na kumtunza vyema kunaweza kusaidia kujitunza pia.

Faida Za Kiafya Za Kuwa Na Mnyama Wa Nyumbani

Athari ya kutuliza ya kuwa na mnyama wa nyumbani unaye penda kunaweza kusaidia kudhibiti uchungu na kupona kwa kasi baada ya upasuaji, kulingana na utafiti.

Utapata usiku mwanana

faida za kiafya za kulala mchana

Kubali paka ama mbwa wako akae chumbani mwako na bila shaka utafurahia usiku usio na bugdha, walisema watafiti kutoka zahanati ya Mayo Clinic Arizona. Lakini hakikisha kuwa mnyama wako wa nyumbani hajifunikii blanketi sawa. Huenda ukapata mzio. Utafiti wa hivi majuzi uligundua kuwa wenye wanyama hawa wa nyumbani hulala vyema zaidi kwa sababu wanahisi fariji na usalama kutokana na wanyama wao kulala karibu nao usiku.

Utahisi furaha zaidi

Kutembeza mbwa wako kunaweza kufanyia mengi kwa afya yako ya kiakili kulingana na wana saikolojia katika Chuo Kikuu cha Liverpool. Wakati ambapo wenyewe wanaweza sisitiza kupata faida hizi, kuwatembeza wanyama hawa kumedhibitika kuboresha mhemko wako, kulingana na utafiti.

Utalinda moyo wako

Kuwa na mbwa kuna husishwa na hatari iliyo punguka ya maradhi ya moyo. Huku ni kulingana na masomo yaliyo fanyika na the Kituo cha Moyo cha Umarekani. Sababu ni ipi? Kutembeza mbwa wako kila siku kunaongeza viwango vyako vya utendaji kazi, na kuwa na athari ya ulinzi kwenye moyo wako. Lakini sio yote kuhusu mbwa: wanyama wa nyumbani wa aina zote huwaegemeza wenyeji wao kijamii. Na kuwasaidia kudhibiti mawazo mengi na kuwahimiza kufuata mitindo yenye afya ya maisha.

Utapata marafiki wapya

Umuhimu Wa Kuishi Na Wanyama Wa Nyumbani

Zaidi ya nusu yetu husema kuwa walio na mbwa huwa wakarimu kuliko kiwango cha wastani. Asilimia 46 wana amini kuwa kuwatembeza mbya ni mojawapo ya njia za kupata marafiki wapya. Na asilimia 29 ya wenyeji wa mbwa husisitiza kuwa wame tengeneza marafiki wa muda mrefu wanapokuwa nje wakitembeza mbwa. Hiyo ni kulingana na utafiti wa 2015. Ni kawaida sana kwa tu wengi kutangamana wanapo ongea kuhusu mapenzi yao kwa wanyama.

Utakuwa na kasi ya miguu

Faida zaidi ya kumtembeza mnyama wako wa nyumbani, ni kuwa utaweza kutembea vyema zaidi. Kulingana na masomo yaliyo fanyika katika Chuo Kikuu cha Missouri, kikundi cha watu wazima kilihimizwa kutembea nje ya nyumba kwa angalau lisaa limoja mara 5 kwa wiki. Walio tembeza mbwa wao wali imarisha uwezo wao wa kutembea, ujasiri na kasi kwa asilimia 28 baada ya wiki 12.

Utadhibiti uzito wako

Faida nyingine ya kumtembeza mbwa wako ni kuwa utachoma kalori katika mchakato huo. Watu walio wa tembeza mbwa wao kwa dakika 20, mara 5 kwa wiki, walipoteza kilo 7.2 kwa mwaka mmoja, kulingana na somo lililo chapishwa mwaka wa 2010.

Faida zingine za kuwa na mnyama wa nyumbani ni kama vile:

  • Kupunguza uchungu wako
  • Kupunguza shinikizo la damu
  • Kupunguza kolesteroli
  • Kuepusha kiharusi

Je, una ngoja nini? Tafuta mnyama wa nyumbani leo!

Soma PiaUnene Wa Kupindukia Kwenye Watoto: Wakati Ambapo Unapaswa Kuwa Na Shaka

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio