Faida 10 Za Kula Scent Leaf Unapokuwa Na Mimba Kwako Na Mtoto Wako

Faida 10 Za Kula Scent Leaf Unapokuwa Na Mimba Kwako Na Mtoto Wako

Mbali na kukipa chakula chako ladha na harufu ya kupendeza, scent leaf inakusaidia sana unapokuwa na mimba.

Mwanamke anapo pata mimba, mtindo wake wa maisha hubadilika mara nyingi. Haitakuwa rahisi kuwacha vitu ambavyo ulimi wako ulikuwa umezoea na kupenda kwa miaka hiyo yote, ila baadhi ya vyakula lazima vitupiliwe mbali unapokuwa na mimba. Iwapo unashangaa ama ni sawa kula scent leaf unapokuwa na mimba, unapaswa kuelewa kwanza faida za scent leaf unapokuwa mjamzito. Pia, kuna vitu ambavyo unahitajika kufahamu kuhusu kiungo hiki cha chakula. Makala haya yana kufunza yote unayo paswa kujua kuhusu scent leaf hasa unapokuwa mjamzito.

benefits of scent leaf in pregnancy

Unaweza kula matawi ya scent leaf ukiwa na mimba, ila kumbuka kula viwango vidogo

Faida za kula scent leaf unapokuwa na mimba: Je, scent leaf ni nini?

Scent leaf ni aina ya mmea unaotumika kwenye supu na vyakula kuongeza ladha na harufu ya kupendeza. Unapatikana katika sehemu zilizo na joto Afrika. Jina lake la kisayansi ni Ocimum Gratissimum. Wana efiks wanafahamu mmea huu kama ntong, wana Igbos wana uita nchanwu, na wana Yoruba kuuita efirin.

Ni rahisi kuukuza, na una patikana katika mashamba mengi ya nyumba. Unaweza panda shina na litaanza kukua baada ya wiki mbili.

Matumizi ya scent leaf

Scent leaf inatumika vyema kwenye supu kama vile egusi, supu nyeusi na okro. Ni kiungo muhimu kwenye mapishi ya nyama ya mbuzi, supu ya kuku wa pilipili na supu ya nyama ya pilipili. Baadhi ya watu hawawezi kula supu yao ikiwa hawaja ongeza kiungo hiki.

Scent leaf freshi ina harufu inayo karibiana na ya basil. Unaweza hifadhi kiungo hiki kwa kukikausha na kukitumia kikiwa kimekauka.

Faida za virutubisho za scent leaf

benefits of Scent Leaf In Pregnancy

Unahitajika kujua uwezo na faida za matawi haya iwapo unakusudia kuyala, kwa sababu unataka faida zake zote unapokuwa na mimba.

Scent leaf ina wingi wa:

  • Kalisi
  • Iron
  • Phosphorus
  • Vitamini A
  • Na potassium

Hapa kuna faida 10 za kula scent leaf unapokuwa na mimba

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

Watu wengi Afrika wanapenda ladha na harufu ya scent leaf, ila hukujua kuwa ina faida nyingi za kiafya kwa wanaume na wanawake? Hapa kuna baadhi ya faida za kupendeza za scent leaf:

1. Kuto chakata chakula (indigestion) na matatizo mengine ya tumbo

Scent leaf inatuliza matatizo mengi ya tumbo. Unaweza ongeza matawi machache kwenye maji moto na utengeneze chai. Chai hii inaweza saidia kupunguza ishara za kuendesha, kukosa maji mwilini na kuto chakata chakula tumboni.

2. Scent leaf inapunguza kisukari

Kuna utafiti unao onyesha matumizi ya scent leaf katika kupunguza kisukari. Watu wanao tatizika kutokana na kisukari cha Non-Insulin wanaweza tumia matawi haya kupunguza kisukari na kulinda pancreas.

3. Uwezo wa antifungal na antibacterial

Scent leaf ina uwezo wa antibacterial na antifungal. Mojawapo ya sababu kwa nini inatumika kama antibacteria ni kwa sababu ya uwezo wake wa kukumbana na vitu kama mbu. Kwani viumbe kama hivi vinabeba viini, na haviwezi karibia mahali ambapo matawi ya scent leaf yako kwa sababu ya harufu yake kubwa.

4. Uwezo wa anti-inflammatory

Scent leaf ina wingi wa kalisi na kuifanya iwe nzuri katika afya ya mifupa. Kuila mara kwa mara huenda kukasaidia kuepuka osteoporosis na mifupa kukosa nguvu. Watu wanao kuwa na tatizo la arthritis wanaweza faidika kutokana na kuongeza scent leaf kwenye lishe zao ama kuinywa kwenye chai.

Kuna faida zaidi za kula scent leaf unapokuwa na mimba

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

5. Inaboresha uzazi kwa wanaume

Faida za scent leaf unapokuwa na mimba huanza kabla ya kutunga. Ina euganol na epigenin fenkhona, inayo saidia kuboresha tendo la ngono kwenye wanaume. Pia inaweza saidia wanaume wanao tatizika na kumwaga mapema. Pia inaboresha utoaji wa manii na wingi wake.

6. Ina imarisha afya ya macho

Vitamini A iliyo kwenye scent leaf ina ifanya kuwa bora kwa afya ya macho. Unaweza ponya conjuctivitis ama Apollo, punguza shinikizo la juu la macho na kuepusha kuto ona usiku.

7. Scent leaf ina tumika kukumbana na harufu mbaya ya mdomo

Ungependa kutoka nyumbani baada ya kula kitu chenye harufu? Kula scent leaf ili unukie vizuri. Watu wanao tatizika na halitosis wanaweza kumbana na hali hii kwa kuiongeza kwenye lishe yao.

8. Ina badilisha athari mbaya za uvutaji sigara

Uvutaji sigara husababisha athara za muda mrefu. Wizara Kuu Ya Afya inawaonya wavutaji sigara kuwa huenda wakafa wangali wachanga. Watu walio wacha kuvuta sigara wanaweza tumia scent leaf kurudi katika maisha yenye afya.

9. Scent leaf ina hutumika kufukuza mbu

Iwapo unaishi sehemu ambazo zina mbu wengi na kutatiza usingizi wako na huenda hata ukaugua malaria, scent leaf itakusaidia kufukuza mbu kwani haziwezi kaa mahali penye harufu.

10. Utoaji wa maziwa

Bado unaweza furahia faida za scent leaf baada ya kujifungua. Mama wanao nyonyesha wanao tatizika na utoaji mdogo wa maziwa wanaweza kunywa scent leaf kwenye chai kuboresha kiwango cha maziwa wanacho toa.

Je, unaweza tumia scent leaf ukiwa na mimba?

Scent leaf ina afya ukiwa na mimba, ila unapaswa kula viwango vinavyo faa. Furahia faida za kiafya za mmea huu unapokuwa na mimba. Walakini, wanawake wenye mimba wanapaswa kukaa mbali na mafuta ya scent leaf kwani ni uwingi usiofaa.

Kumbukumbu: NHS

Guardian.ng

Soma pia: 3 things you need to know about carbs during pregnancy

Written by

Risper Nyakio