Chakula sahihi cha kumpatia mtoto anayeanza kula ni moja ya mambo muhimu ambayo huwasumbua wazazi wengi. Kwa kawaida, mtoto kuanzia umri wa miezi sita huanza kupewa uji maalum kama kianzio cha kujifunza kula. Uji wa muhogo kwa mtoto huwa ndio chaguo la wengi. Soma zaidi kuhusu faida za uji wa muhogo kwa mtoto.
Kwa Nini Uji wa Muhogo Kwa Mtoto?

Muhogo ni zao la mzizi. Ni zao maarufu sana kwa sababu linavumilia ukame na kustawi vizuri bila ya kuhitaji mbolea. Hili zao limefahamika vizuri sana kwa sababu muhogo na unga wa muhogo ni chanzo kizuri na rahisi cha wanga.
Watu huandaa na kula chakula cha muhogo kwa njia mbalimbali katika sehemu mbalimbali za dunia. Kuoka, kuchemsha, na pia watu huvundika na kutumia katika mfumo wa unga.
Unga salama wa mtoto ni ule ambao hauja kaa muda mrefu, hauna mchanganyiko wa vitu vingi sana, na uwe umezingatia vipimo vya kila kiungo. Muhimu pia ni kuhakikisha nafaka unazo weka zimeandaliwa vizuri hazija vunda, zimeoshwa vizuri na kukauka.
Faida Za Uji Wa Muhogo Kwa Mtoto
- Ni chakula chenye kalori nyingi zaidi kuliko mazao mengine ya mizizi na majani
- Pamoja na kuwa muhogo una protini nyingi na mafuta kwa kiasi kidogo kuliko mazao ya nafaka, bado kiwango hiki ni kikubwa kuliko cha mazao mengine ya mizizi
- Muhogo hauna kemikali iitwayo gluten ambayo inaweza kusababisha athari za magonjwa kwa mlaji
- Majani machanga ya muhogo hutumika kutengeneza mboga aina ya kisamvu. Huwa chanzo kizuri cha protini na vitamini K. Vitamin K huimarisha mifupa
- Muhogo ni chanzo kizuri cha vitamini C, thiamine, riboflavin na niacin, madini ambayo ni muhimu sana katika utendaji murua wa mwili wako
- Madini kama vile chuma, potasiamu, zinki, magnesiamu,shaba na manganizi hupatikana kwa wingi katika chakula cha muhogo
Je, Muhogo Huwa Na Sumu?

Hupaswi kula muhogo mbichi kwa sababu una aina mbili za sumu ya cyanide. Kuupika na kuuloweka muhogo kwa ajili ya kuandaa unga wa uji ama ugali huondoa sumu hiyo. Kula chakula hiki pasipo kuandaliwa vyema au kwa namna isiyo sawa kunaweza kusababisha athari mbaya za kiafya.
Hata hivyo, bidhaa zinazotokana na zao la muhogo kama vile unga ni salama kuliwa kwa kupikwa. Hii ni kwa sababu tayari sumu inakuwa imeondolewa kupitia jua au kulowekwa na kuanikwa juani.
Madhara makubwa yanayoweza kutokana na kushindwa kuandaa vyema uji wa mtoto ni:
- Nafaka zikiwa chafu mtoto ataharisha. Na ikitokea mahindi au nafaka nyingine yoyote ilikuwa na dawa na ukapika bila kuosha vizuri mtoto anaweza pata matatizo ya ini
- Pia nafaka ambazo hazikukauka vizuri mfano yaweza kuwa karanga, mahindi au yoyote ikivunda kuna sumu ambayo inaitwa flatoxin inapatikana humo inaweza pia leta tatizo la ini
- Kama kiwango cha wanga kimezidi sana unampa mtoto nguvu nyingi ambayo haitaji kwa muda huo. Na kwa mtoto mwenye kisukari ukimpa uji wenye wanga mwingi lazima sukari itakuwa inapanda.
Kupata mtoto ni safari mpya wazazi huanza kupitia, ni kipindi ambacho hubadilisha maisha na mipango ya wazazi. Chaguo la uji wa muhogo kwa mtoto wako ni bora kwa sababu ya manufaa mengi kwa afya yake. Faida za uji wa muhogo kwa mtoto ni nyingi na muhimu katika ukuaji na maendeleo yake.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Chakula Bora Cha Mtoto Wa Miezi Tatu