Nambari ya wanawake wanaotumia uzazi wa mpango imeongezeka kutoka milioni 900 katika mwaka wa 2000 hadi bilioni 1.1 katika mwaka wa 2020. Makadirio yanaonyesha kuwa wanawake milioni 70 zaidi watakuwa wanatumia uzazi wa mpango katika mwaka wa 2030. Faida za uzazi wa mpango sio kwa mwanamke pekee, mbali kwa jamii kwa jumla. Tunaangazia athari za kutumia njia za kupanga uzazi.
Faida za uzazi wa mpango

1.Kupunguza nambari ya kuavya mimba kusiko salama
Kutumia uzazi wa mpango kama utumizi wa tembe na kondomu kunasaidia kulinda dhidi ya kupata mimba isiyohitajika. Wanawake wanaopata mimba isiyohitajika hukua katika hatari ya kuavya mimba kwa kutumia mbinu zisizo salama. Kuavya mimba nje ya vituo visivyo na vyeti vya kufanya hivyo huwaweka wanawake katika hatari ya kupoteza maisha yao.
2. Kuboresha afya ya mama
Mbinu za uzazi wa mpango hulinda dhidi ya kupata mimba kabla ya mama kuwa tayari. Kwa sababu hii, anaweza kuyapanga maisha na afya yake. Mama anapotumia uzazi wa mpango baada ya kujifungua, kunapunguza hatari za kufariki kwa mama kwa asilimia 35.
3. Kuwawezesha wanawake
Wanawake wanaopanga uzazi wana usemi kuhusu mambo tofauti yatakavyo tokea maishani mwao. Wanaweza kuyapanga maisha yao, wakati wa masomo, wakati wa kazi na kupata vyeo zaidi kazini na wakati mwafaka zaidi kwao kupata watoto.

4. Kulinda dhidi ya maambukizi ya kingono
Kutumia mpira wa kondomu kama njia ya uzazi wa mpango ndiyo njia bora zaidi ya kulinda dhidi ya kupata ukimwi na maambukizi mengineyo ya kingono.
5. Kudhibiti idadi ya watu duniani
Kuwa na watu wengi zaidi duniani huathiri vitu vingi. Ukuaji wa kijamii na kiuchumi watu wanapopigania raslimali chache zilizoko kama chakula, mashule na makazi. Kupanga uzazi kunadhibiti idadi ya watu na kuwapa nafasi ya kutumia raslimali chache zilizoko.
Faida za uzazi wa mpango sio kwa mwanamke tu, mbali kwa jamii, mazingira na dunia yote. Masomo kuhusu uzazi wa mpango yanapaswa kuendelea ili kuwajulisha wanawake hata walio mashinani kuhusu chaguzi zao. Kuwa wanaweza kupanga maisha yao na kufanya uamuzi kuhusu wakati unaowafaa zaidi kuwa wazazi.
Soma Pia: Njia Za Kisasa Za Kupanga Uzazi Na Athari Zake Kwa Mwanamke