Utafiti Unasema Kuwa Familia Zenye Watoto Wawili Huwa Na Furaha Zaidi

Utafiti Unasema Kuwa Familia Zenye Watoto Wawili Huwa Na Furaha Zaidi

Utafiti mpya unaonyesha kuwa familia iliyo na watoto wawili huwa na furaha ikilinganishwa na familia zenye watoto zaidi.

Ushawahi kujiuliza kuhusu familia ya watoto wawili na iwapo unapaswa kuwa na watoto wachache ama wengi zaidi?

Utafiti wa hivi majuzi kwa wanandoa kwa miaka 18 baada ya kujifungua watoto wao. Somo hili lili gundua kuwa “furaha huongeza na miaka kabla na baada ya kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza. Ila hupunguka kwa kasi na kurudi kwa hali yao ya furaha ya kabla ya kujifungua. Watafiti walipata kuwa kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza na wa pili huongeza furaha, ila wa tatu mambo yana badilika. Utafiti ulichapishwa kwenye makala ya Demography na yana habari kuhusu familia za Britain na Germany.

“Matokeo yetu yana onyesha furaha ya muda mdogo kwa wazazi karibu na wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza na wa pili. Ukweli kuwa furaha ya uzazi huongezeka kabla ya watoto hawa kuzaliwa ina ashiria kuwa tuna angazia masuala zaidi ya kujifungua. Kama vile wanandoa kuwa na ushirikiano na kufanya mipango ya siku za usoni,” alisema Mikko Myrskyla. Mikko ni professa wa demographia katika kituo cha LSE na mkurugenzi wa Germany Max Planck Institute for Demographic Research.

Myrskylä aliorodhesha sababu ambazo zingechangia katika kupunguka kwa furaha ambako wazazi hushuhudia baada ya kujifungua mtoto wao wa tatu. Mapitio ya uzazi hupunguka furaha;familia kubwa hushinikiza akiba ya wazazi; uwezekano wa mimba kuto pangwa huongezeka na idadi ya watoto ambao mwanamke anao tayari. “Huku huleta mawazo zaidi,” Myrskyla alisema.

Familia ya watoto wawili: Sababu kwa nini kuwa na watoto wawili ni bora kwa baadhi ya familia

familia ya watoto wawili

 Jina moja: pesa

Watoto ni gharama. Kuwalisha, kuwavisha, na kuhakikisha wana afya, na bado huja angalia majukumu yote. Lazima ushughulikie karo ya shule na kabla ya kuanza shule. Na pia mambo yanayo hitajika kuhakikisha kuwa mtoto wako ana maisha bora, kumnunulia vidoli na nguo. Watoto ni kama benki ndogo. Hii ni kweli kwa nambari yoyote ya watoto, ila ni msukumo mkubwa kwa wazazi wengi kubaki na watoto wawili tu.

Iwapo una lea na mchumba wako, mna sawasisha mambo

Watoto wawili hawawezi tengeneza kikundi na kuwapiku wazazi wao, ambalo ni jambo nzuri. Unaweza kujipanga vyema. Kwa hivyo hauna majukumu mengi zaidi. Huu unapaswa kuwa msukumo wa kukufanya upate watoto wawili tu.

Unaweza tumia vitu vya mtoto wako bila kuvitumia mara nyingi zaidi

Iwapo una pata mtoto wa pili, anaweza tumia vitu ambavyo ndugu yake mkubwa alitumia. Una vitumia kwa miezi mitatu. Wakati ambapo hauwezi kana kuwa vitu hivi ni muhimu, unaweza vitumia kwa mtoto wako wa pili. Kwa hivyo kuna maana ya kuvitumia tena kabla ya vizeeke.

Watoto wazuri

Hapa kuna jambo kuhusu familia ya watoto wawili: kuna ukaribu mkubwa kwani ni wao pekee. Na nyakati zinapokuwa ngumu, hakuna hatari ya kumleta ndugu wa tatu, nne ama wa tano kwenye mapigano haya na huenda yakafanya kuwa na pande. Wakati unapokua mgumu kwa ndugu wawili, ni kati yao tu. Nyakati zinapo kuwa nzuri, ndugu wawili wanapendeza zaidi.

Kuwa tayarisha watoto wako kwa kuwa na familia ya watoto wawili

familia ya watoto wawili

familia yenye watoto wawili

Kupata mtoto mwingine ni mabadiliko makuu kwa mtoto mdogo, na hawaelewi kabisa. Yote wanayo jua ni kuwa mama na baba wanampa mtoto mdogo wakati zaidi. Ili kusaidia kuzoea jambo hili, ni vyema kuanza kuwa tayarisha watoto wakubwa vyema kabla ya kujifungua.

Huffpost

Soma pia: These Husbands Have Found Creative Ways To Tackle Their Pregnant Wife Problems

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio