Haijalishi nambari ya watu utakaozungumza nao ama vitabu utakavyo soma kujitayarisha, hakuna kitakacho kutayarisha vya kutosha kuwa familia ya watoto wawili. Kwa baadhi ya wazazi, jambo gumu zaidi la kupata mtoto wa pili ni kuwa mzazi kamili. Unapokuwa mzazi wa mtoto mmoja, kuna baadhi ya mitindo ya kimaisha ya kabla ya mimba unayokuwa nayo bado. Ila, baada ya kupata mtoto wa pili, maisha yanabadilika kabisa.
Unapokuwa na mtoto mmoja, una wakati wa kulala ama kufanya vitu vingine mtoto anapokuwa amelala. Ila, wanapokuwa watoto wawili, hauna muda kabisa. Hata hivyo, mtoto wa pili huwa na faida zake.
Manufaa ya familia ya watoto wawili

Licha ya changamoto zinazoandamana na kupata mtoto wa pili, mtoto wa pili huwa na manufaa.
Kuwa na watoto wawili humpa mzazi wakati wa kupumzika. Hapo awali alikuwa akihitajika kucheza na mtoto wake wakati wote. Ila sasa, ana ndugu ambaye anaweza kucheza naye.
Kuona watoto wako wawili wakicheza humjaza mzazi na furaha nyingi.
Mzazi anapopata mtoto wa pili, anafahamu jinsi ya kumtunza mtoto na vitu vyote vinavyopaswa kufanywa kwa hivyo yeye sio mgeni. Kumlisha, mfumo wa kulala na kadhalika.
Mtoto wa pili hata hitaji kununuliwa vitu vingi kwani atatumia vitu vilivyo nunuliwa ndugu yake mkubwa.
Kujitayarisha kupata mtoto wa pili

Unapojitayarisha kupata mtoto wa pili, utahitajika kuwa na ratiba spesheli ya wakati, kupanga fedha zako na kujua jinsi utakavyofanya vitu tofauti kwenye nyumba.
Anza kwa kunua vitu utakavyohitaji muda kabla ya kujifungua. Ikiwa nguo ulizo nazo za kifungua mimba chako hazitatosha, anza kwa kununua zingine. Pamoja na diaper na mahitaji mengine makuu.
Ikiwa utahitaji usaidizi kufua na kufanya kazi za kinyumbani, hakikisha kuwa unatafuta msaidizi muda kabla ya kujifungua.
Mabadiliko katika uhusiano baada ya mtoto wa pili

Uhusiano kati ya wanandoa utaadhiriwa. Kuwa na watoto wawili kwenye nyumba kuna maanisha kuwa wana mahitaji zaidi, na watahitaji kutunzwa zaidi. Hii ina maanisha kuwa wazazi hawatakuwa na muda mwingi wa kipekee na bila shaka uhusiano wao utaadhiriwa.
Wazazi wanapaswa kusaidiana hasa katika siku za kwanza. Pia, wanandoa wanastahili kuhakikisha kuwa wanapaswa kuzungumza kuhusu hisia na mawazo yao.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Mapumziko Kabla Na Baada Ya Kujifungua Yana Umuhimu Upi Kwa Mama?