Mitindo Ya Mavazi Ya Agbada Inayo Vuma Zaidi

Mitindo Ya Mavazi Ya Agbada Inayo Vuma Zaidi

Mitindo inayo vuma ya Agbada unayo paswa kuhakikisha uko nayo!

Hapo awali, mtindo huu wa female agbada gown styles ulikuwa gauni mrefu zilizo valiwa na wanaume wakienda sherehe spesheli ama mahali rasmi. Ila leo, mtindo huu umebadilika na hata kama umaarufu wake ulianza huko nchi ya Nigeria, leo hii unavaliwa na watu wa nchi mbali mbali Afrika kote. Na pia wanawake pia wanavalia mavazi haya.

Mwanzoni nguo hizi zilikuwa ishara ya utajiri na kutambulika kwenye jamii na pia kujivunia utamaduni wa jamii yako. Mara nyingi mavazi haya hufika kwenye goti. Lakini wanawake wameanza kuvalia mavazi haya na kuleta mitindo mipya ambayo imevuma sana.

Jinsi Ya Kuvalia Mavazi Ya Agbada Ya Wanawake

mitindo ya agbada ya kike

Mavazi haya ya female agbada gown styles hata kama mwanzoni ilikuwa ya wanaume, siku hizi wanawake ndio wanajulikana kuivalia sana. Mavazi haya yana weza valiwa kwenda mahali popote, kwenda kazini, kanisani ama hata kwenda kwa sherehe. Kuna njia tofauti za kuvalia mavazi haya. Unaweza valia ikiwa kama blausi ama gauni mrefu. Makala haya yana kuelimisha kuhusu njia tofauti unaweza valia agbada yako na mapambo, ili upendeze kuenda mahali popote pale. Ni vyema kukumbuka kuwa mapambo unayo valia na nguo yoyote ina lingana na mahali unapo enda. Huenda ikawa sio sawa kwenda kazini na mikufu na herini ndefu.

Kumbuka kuambatanisha mapambo yako na mahali unapo enda siku hiyo.

Vidokezo muhimu vya kukumbuka unapo valia vazi lako la agbada

Agbada ankara gowns

Chanzo: Afrocosmopolitan.com

Kuna siku ambazo vazi hili lilikuwa lime hifadhiwa wanaume kwa jamii peke yake. Ila na mabadiliko katika mitindo ya mavazi, vazi hili lina valiwa kwa sherehe za kila siku na wanaume kwa wanawake. Huenda ukawa na shaka za jinsi ya kuvalia vazi hili ili liandamane na mahali unapo enda. Ni vyema kukumbuka mambo haya.

Vazi hili linaweza valiwa na kila mtu. Hata watoto wako. Kuna picha nyingi kwenye mtandao za familia ikivalia agbada inayo fanana. Kwa hivyo kama una watoto, usione haya kuwashonea agbada sawa na yako mara ijayo unapo enda kwa fundi wako wa mitindo. Mtapendeza sana, hasa mnapo enda kujumuika na sherehe ya kifamilia.

Chagua rangi inayo vutia. Mara nyingi, watu hukosa kujua rangi inayo andamana na ngozi yao na kuwavutia zaidi. Kununua vazi ya rangi isiyo kufaa huenda kukakufanya uchukie kuvalia nguo fulani. Shida sio nguo uliyo nunua, ila rangi na nguo hiyo. Kwa agbada, vazi lenye rangi inayo ng’aa ina shauriwa.

Naweza valia nini na Agbada. Unaweza amua kushona agbada yako ikiwa blausi na suruali ama blausi kisha kuvalia na suruali tofauti unazo valia siku zingine.

Mitindo tofauti ya Agbada

Blausi: Unaweza amua kushona blausi peke yake. Kuna mitindo tofauti ya kushona blausi. Kuna aina inayo kuwa mrefu kana kwamba rinda, ila fupi kuliko rinda. Unaweza valia peke yake msimu wa jua. Ama unaweza valia na suruali nyeusi ikiwa blausi yako ya Agbada ni ya rangi inayo ng’aa.

Gauni na suruali: Huu ni mtindo maarufu sana unapo shona Agbada ya rangi sawa blausi na suruali. Hauna shaka ya utakacho kivalia na Agbada yako. Mtindo huu unakufanya kukaa rasmi zaidi na kupendeza ikiwa unaenda sherehe rasmi.

Rinda: Badala ya kuendea blausi na suruali ambazo ni maarufu sana, unaweza vunja sheria na uvalie rinda la kibinafsi lililo tofauti na mavazi mengine. Unaweza valia rinda hili kwenda kazini ikiwa urefu wake unakubalisha. Ama kwenda kwenye sherehe zozote zile.

Kuna njia tofauti ambazo unaweza tengeneza agbada yako. Tuna tumai vidokezo tulivyo angazia vya female agbada gown styles vitakusaidia unapo amua kuongeza vazi hili kwenye sanduku lako la mavazi.

Soma pia:Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio