Tunakuja Afrika! Fenty beauty itakuwa Africa.

Mwimbaji mashuhuri na mwanabiashara Robyn Rihanna Fenty mmliki wa biashara ya Fenty Beauty na Fenty Skin ametangaza kuwa bidhaa zao zitakuwa Afrika.
Katika tarehe 8 mwezi wa September mwaka wa 2017, Rihanna alianzisha biashara ama brand ya Fenty Beauty. Ina husika na urembo na mapodizi na sio kwa wanawake tu. Inafahamika kwa sana katika bara zote kwani ina husisha aina zote za ngozi na jinsia. Tarehe 24 Mei, walifungua duka lao la kwanza huko Paris kisha wakaendelea kufungua maduka katika maeneo tofauti duniani kote.
Picha: Badgirlriri Instagram
Katika chapisho lake kwenye kurasa yake Instagram, Rihanna Fenty ametangaza kuwa wanafungua maduka katika Afrika.
Alisema, “Nimekuwa nikingojea muda huu!! Fenty Beauty na Fenty Skin zitakuwa Afrika!!!
Botswana, Ghana, Kenya, Namibia, Nigeria, South Africa, Zambia, Zimbabwe.. Tunakuja kwenu Mei tarehe 27 na huo ni mwanzo tu!!! Alidokeza.
Picha: Fentybeauty Instagram
Habari hizi zimepokeleka kwa furaha na wafuasi wake kutoka bara la Afrika. Wengi ambao hapo awali walikumbana na matatizo walipotaka kununua bidhaa kutoka kwa maduka haya.
Picha: Fentyskin Instagram
Licha ya kuwa mjamzito, mwimbaji huyu anazidi kuikuza biashara yake na ni jambo la kutia moyo. Hongera Rihanna kwa hatua hii kubwa ya kufungua fenty beauty Africa. Bila shaka watu wengi wataweza kupata bidhaa zake kwa urahisi zaidi.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Corazon Kwamboka: Jinsi Ya Kuwa Mzazi Bora Wa Kipekee