Fibroids ni aina ya vidonda visivyo sababisha saratani ambavyo hukua kwenye uterasi. Vidonda vya fibroids katika mimba vinaweza kutolewa ama kudhibitiwa kwa kupitia upasuaji ama kuchukua dawa za kupanga uzazi. Katika kesi sugu, mwanamke anaweza kushauriwa kufanyiwa upasuaji.
Manufaa

Faida za upasuaji kutoa fibroids kuna lingana na aina ya upasuaji ambao mwanamke alifanyiwa. Kuna aina tofauti za upasuaji ambazo zinatumika kutoa vidonda vya aina hii kwa uterasi ya mwanamke. Baadhi ya manufaa ni kama vile:
- Kupunguka kwa uchungu ama shinikizo
- Kutoa vidonda vya fibroids mwilini
- Kupunguka kwa kuvuja damu
Hatari
Idadi kubwa ya watu ambao wanafanyiwa upasuaji wa kutoa vidonda vya fibroids kwenye uterasi hawapati matatizo sugu. Lakini mara nyingi, watashuhudia kuvuja damu na huenda wakahitaji muda kupona. Kwa kesi sugu, huenda waliofanyiwa upasuaji waka tatizika kutokana na hatari hizi:
- Maambukizi
- Upasuaji kuto fuzu
- Kuugua maambukizi
- Kuvuja damu nzito
- Vidonda vya fibroids kukua tena
- Uterasi kuathiriwa katika mchakato wa upasuaji
Upasuaji wa fibroids una athari kwa uwezo wa uzalishaji wa mwanamke

Athari za upasuaji wa kutoa fibroids zina lingana na aina ya upasuaji uliofanyika. Kuna aina ya upasuaji usio mwezesha mwanamke kuweza kujifungua tena. Kama vile upasuaji wa endometrail ablation na hysterectomy. Huku aina za upasuaji za morcellation, radio frequency ablation na embolization zikimwezesha mwanamke kujifungua.
Uponaji
Huenda mwanamke aka hitajika kulala hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa fibroids. Mwanamke anaweza jaribu mambo haya ili kutuliza uchungu baada ya upasuaji wa aina hii.
- Kumwuliza daktari kuhusu muda wa uponaji wa aina hasa ya upasuaji alio fanyiwa
- Kufuata kwa makini maagizo aliyo patiwa na daktari ili apone kasi
- Kupata usaidizi kufanya kazi za kinyumbani, kutoka kwa wanafamilia na marafiki siku chache baada ya kutoka hospitalini
Sawa na aina zingine za upasuaji, upasuaji wa kutoa fibroids unawasaidia wanawake wanao tatizika na aina hii ya vidonda. Na kuwasaidia kuwa na ubora zaidi wa kiafya.
Ni vyema kufanya utafiti na kuwasiliana na wataalum katika nyanja hii kabla ya kufanya uamuzi kuhusu aina ya upasuaji utakao fanya kudhibiti fibroids katika mimba.
Soma Pia :Aina Ya Maumivu Ya Matiti Yanayo Ashiria Ujauzito: Aina Na Matibabu Yake!