Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Fibroids Na Mimba: Hatari Za Fibroids Kwa Mimba

3 min read
Fibroids Na Mimba: Hatari Za Fibroids Kwa MimbaFibroids Na Mimba: Hatari Za Fibroids Kwa Mimba

Fibroids na mimba huwatia wajawazito wengi shaka, ila, kufuatia maendeleo katika nyanja ya afya, kuna mengi yanayoweza kufanyika na mama kujifungua salama.

Fibroids na mimba, je kuna uhusiano upi? Fibroids ni aina ya vidonda visivyo vya saratani vinavyokua kwenye tumbo la uzazi. Ni kawaida kwa wanawake wengi kupata fibroids katika kiwango kimoja maishani mwao. Hasa katika miaka yako ya kupata watoto. Fibroids hazina athari na mara nyingi huisha kabla ya kujulikana, hata hivyo, katika visa nadra, huenda vikaathiri uwezo wa mwanamke wa kujifungua na ujauzito.

Fibroids na mimba

fibroids na mimba

Idadi kubwa ya wanawake haiathiriwi na kuwepo kwa fibroids katika ujauzito. Asilimia ndogo ya kati 10 na 30 ya wanawake wanaopata fibroids na mimba huenda wakapata matatizo katika ujauzito wao. Hasa kufuatia uchungu unaoandamana na kuwepo kwa fibroids.

Hatari zinazohusika na kuwa na fibroids katika ujauzito na kujifungua

1.Kujifungua kabla ya wakati. Uchungu mwingi unaoandamana na kuwa na fibroids huenda ukasababisha mikazo  ya uterasi na kusababisha kujifungua kabla ya wakati.

2. Kutokua kwa fetusi. Iwapo fibroids ni kubwa, huenda zikatatiza ukuaji wa mtoto kufuatia nafasi iliyopunguka ya kuhimiza ukuaji wa mtoto.

3. Kujifungua kupitia upasuaji wa c-section. Wanawake walio na vidonda vya fibroids watahitaji kujifungua kupitia upasuaji zaidi ikilinganishwa na wanawake wasio na vidonda hivi.

4. Kupoteza mimba. Kulingana na utafiti, nafasi za mwanamke kupoteza mimba anapokuwa na fibroids zimeongezeka kwa mara mbili.

5. Mtoto kuwa breech position. Kwa sababu tumbo la uzazi lina shepu isiyo ya kawaida, mtoto huenda akakosa kuwa kwa position anayohitajika anapojifungua.

Ishara za fibroids

  • Vipindi vya hedhi vyenye uchungu zaidi
  • Kuhisi uchungu katika tendo la ndoa
  • Uchungu kwenye mgongo
  • Kuvimbiwa
  • Kuvuja damu kati ya vipindi vya hedhi
  • Vipindi vya hedhi vinavyodumu muda mrefu
  • Matatizo ya uzalishaji kama kutatizika kujifungua, kujifungua kabla ya wakati ama kuharibika kwa mimba
  • Kukosa damu tosha mwilini kufuatia kupoteza damu nyingi

Matibabu ya fibroids katika ujauzito

fibroids na mimba

Matibabu ya fibroids katika ujauzito huwa imedhibitiwa kwa sababu ya hatari ya kuathiri fetusi. Mara nyingi, mwanamke aliye na fibroids katika mimba hushauriwa kupumzika, kunywa maji tosha ama kupatiwa dawa za kupunguza uchungu. Mwanamke anapofika katika muhula wa pili wa mimba, huenda akafanyiwa upasuaji wa myomectomy kutoa fibroids bila kugusa tumbo la uzazi.

Athari za fibroids kwa uzalishaji wa mwanamke

Wanawake wengi wanaweza kupata mimba kwa njia asili hata wanapokuwa na fibroids bila kutumia matibabu yoyote. Katika visa vingine, huenda uzalishaji wa mwanamke ukaathiriwa na kuifanya iwe vigumu kwake kutunga mimba ama kupoteza mimba.

Kuwepo kwa fibroids kwenye uterasi ya mwanamke kunaweza kudhibitika katika kipimo cha pelviki ama ultrasounds. Fibroids na mimba sio chanzo cha shaka, wasiliana na daktari kuhakikisha kuwa mimba inakua ipasavyo.

Chanzo: Medicalnewstoday

Soma Pia: Mapumziko Ya Kitanda Katika Mimba Na Athari Hasi Kwa Mama

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Fibroids Na Mimba: Hatari Za Fibroids Kwa Mimba
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it