Fibroids Zina Athiri Uwezo Wako Wa Kupata Mimba?

Fibroids Zina Athiri Uwezo Wako Wa Kupata Mimba?

Fibroids nyingi hazibadili saizi katika ujauzito, lakini zingine hubadilika.Ukuaji wako wa estrogen una athiriwa na estrogen inayo ongezeka katika ujauzito.

Fibroids ni vitu ambavyo vinakua kwenye kuta za uterasi na ambazo hazi sababishi saratani. Ni maarufu sana na kama una fibroids, huenda uka jiuliza kama kuna uwezekano kwako kuanzia familia ama zita sitisha mipango yako ya kuwa mama. Fibroids zina zuia mimba? Tuna fahamu zaidi kwa makala haya.

Fibroids zina zuia mimba? Kivipi?

fibroids zina zuia mimba

Wanawake wengi walio na fibroids hawata shuhudia athari zozote kwenye mimba yao. Wataendelea na kujifungua watoto warembo na wenye afya. Lakini utafiti uliofanyika 2010 una shauri kuwa asilimia 10 hadi 30 ya wanawake walio na fibroids huwa na changamoto kwenye mimba yao. Watafiti wanasema kuwa athari maarufu zaidi ni uchungu.  Hasa kwa wanawake walio na fibroids zaidi ya sentimita 5 walio katika trimesta mbili za mwisho.

Fibroids huenda zikaongeza hatari yako ya matatizo mengine katika ujauzito na kujifungua. Hizi ni kama vile:

  • Kuzuia kukua kwa fetusi. Fibroids kubwa huenda zika zuia fetusi yako kuto kua ipasavyo kufuatia chumba kidogo kwenye uterasi.
  • Kuathiri placenta. Kuna fanyika pale ambapo placenta ina toka kwenye kuta za uterasi kwa sababu ina zuiwa na fibroids. Huku kuna punguza hewa na virutubisho.
  • Kujifungua kabla ya wakati. Uchungu kutokana na fibroids huenda uka sababisha uterasi kubana na kusababisha kujifungua mapema.
  • Kujifungua kupitia upasuaji. Wataalum wanasema kuwa wanawake walio na fibroids wako katika nafasi ya mara hadi 6 ya kujifungua kupitia upasuaji wa c-section ikilinganishwa na wanawake wasio na hali hii ya afya.
  • Kupoteza mimba. Utafiti una dhihirisha kuwa nafasi za kupoteza mimba zina ongezeka kwa wanawake walio na fibroids.

Fibroids zinaweza kuathiri uzalishaji?

fibroids zina zuia mimba

Fibroids nyingi hazi athiri, lakini zingine zinaweza- kulingana na saizi yake na mahali zilipo- huenda zika athiri uwezo wa manii kufikia yai. Na kuathiri mchakato wa kurutubishwa kwa yai ama yai kupandikiza kwenye kuta za uterasi. Fibroids huenda pia zika athiri ujauzito kulingana na mahali zilipo kwenye uterasi ambapo mtoto ana stahili kuwa. Mara nyingi, madaktari wata shauri kuwacha fibroid ilipo na kuangalia ujauzito wako kwa umakini.

Athari za ujauzito kwa fibroids

Fibroids nyingi hazibadili saizi katika ujauzito, lakini zingine hubadilika.Ukuaji wako wa estrogen una athiriwa na estrogen na viwango vya estrogen mwilini vina ongezeka ukiwa na mimba. Na kufanya fibroids zikue. Ila kwa wanawake wengine, huenda fibroids ika punguka katika mimba. Utafiti ulio fanyika mwaka wa 2010, uli dhihirisha kuwa asilimia 79 ya fibroids zilizoko kabla ya mimba hupungua kwa saizi baada ya kujifungua.

Soma Pia: Vidokezo Vya Kuwa Mama Mwema Kwa Watoto Wako: Sifa 5 Za Mama Mwema

Written by

Risper Nyakio