Mwili hutatizika kumeng'enya wanga unaopatikana kwenye vyakula tofauti. Lakini bakteria tumboni mwako hufanya kazi ya uchakataji. Ni vyakula gani vinavyosababisha gesi kujaa tumboni?
Vyakula vinavyosababisha gesi kujaa tumboni
Vyakula vyenye mafuta nyingi

Vyakula vilivyo na ufuta mwingi hupunguza mchakato wa chakula tumboni. Nyama zenye mafuta nyingi huwa na asidi nyingi na sulfur. Bakteria zinazomeng'enya nyama tumboni huvunja sulfur na kutengeneza sulfide hydrogen. Na kisha kuongeza gesi tumboni.
Vitunguu

Ulaji wa vitunguu hasa vitunguu saumu huongeza gesi mwilini na kufanya tumbo kujaa. Ni muhimu kuwa makini na viwango vya vitunguu saumu unavyochukua.
Mayai

Kuna baadhi ya watu wanaoathiriwa na gesi wanapokula mayai. Mayai huwa na sulphur. Ikiwa unaathiriwa na gesi unapokula mayai, ni vyema kujitenga na ulaji wa mayai kabla ya kuzungumza na daktari wako.
Bidhaa za maziwa

Bidhaa za maziwa huwa na viwango vikubwa vya lactose, hasa maziwa ya mbuzi na ng'ombe. Kuwa na viwango vikubwa vya lactose mwilini hufanya iwe vigumu kuichakata mwilini. Kisha kusababisha kuwa na gesi kujaa tumboni.
Kabeji na broccoli

Mboga za majani kama vile kabeji na broccoli zinapoliwa na kuchakatwa mwilini hutoa sulphur zinapochakatwa. Inayochangia pakubwa katika kuongeza gesi tumboni.
Ngano na nafaka

Bidhaa za ngano kama vile mkate, pasta na nafaka zingine huenda zikasababisha maumivu ya tumbo. Hii ni kwa sababu bidhaa za ngano huwa na fructans zinazosababisha gesi tumboni ama kufanya tumbo kujaa.
Matunda
Baadhi ya matunda kama vile tufaha na maembe huwa na fructose nyingi na pia nyuzinyuzi nyingi. Huwa vigumu kwa mwili kumeng'enya fructose ama sukari zaidi mwilini. Ila luctose ni ngumu zaidi kumeng'enya ikilinganishwa na fructose.
Jinsi ya kutatua suala hili
- Kunywa chai ya tangawizi
- Kunywa glasi moja ya sharubati ya limau
- Kufanya mazoezi kama vile kutembea
- Kutafuna chakula kwa utaratibu ili kuepuka kuwa na gesi nyingi tumboni
Mara nyingi tatizo la gesi kujaa tumboni huisha bila matibabu yoyote. Tumbo kujaa hupungua baada ya siku chache. Lakini tatizo hili linapozidi kwa siku nyingi bila kuwa bora, ni vyema kuwasiliana na daktari.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Manufaa Ya Kula Kitunguu Saumu Kwa Afya Yako