Gharama ya huduma za uja uzito kwa mama mwenye mimba nchini Kenya

Gharama ya huduma za uja uzito kwa mama mwenye mimba nchini Kenya

Huduma za uja uzito ni muhimu kwa mama mja mzito na mtoto aliye mbeba tumboni. Ana paswa kuanza huduma hizi punde tu anapo gundua kuwa ana mimba. Je huduma hizi ni ghali nchini?

Huduma za uja uzito ni muhimu sana kwa mama mja mzito.  Ni muhimu kwa kila mama mja mzito kujua gharama ya huduma za uja uzito. Zina saidia wauguzi kufuatilia afya ya mama na ya mtoto aliye tumboni na kuhakikisha kuwa wote wako salama na bila ya magonjwa ama matatizo yoyote. Mama mja mzito anashauriwa kufuata huduma hizi na kuhakikisha kuwa anamwona daktari baada ya muda mchache. Iwapo anahisi maumivu yotote mwilini pia ni vyema amjulishe daktari wake. Katika wakati huu, anapewa virutubisho vinavyo msaidia na mtoto wake kukua kwa njia inayo faa. 

Inasemekana kuwa asilimia 21 ya wana wake waja wazito wana aga dunia kila siku nchini Kenya. Hili ni jambo la kusikitisha sana na lina fanya idadi ya watoto wachanga wanao zaliwa nchini kupunguka kwa sana. Idadi hii ni sawa na mabasi mawili yanayo tumika nchini Kenya kuwasafirisha abiria. Hii ni kufuatia wana wake hawa Kutopata huduma bora za uja uzito.  Ama wanawake hawa kukosa kufika hospitalini kwa wakati. Ili wapate usaidizi wa madaktari na wauguzi wanapo jifungua. Hapo awali idadi ya hospitali za wamama waja wazito kujifungulia zilikuwa chache sana. Kwa sasa, serikali ya Kenya imefanya jitahada nyingi kuhakikisha kuwa kuna hospitali ama vituo vya matibabu sehemu mbali mbali. Na pia inawasaidia wamama kutotembea muda mrefu kupata huduma za uja uzito ama ili wajifungue.

Gharama ya huduma za uja uzito

Wataalum wa afya nchini wana wahimiza wamama waja wazito kupata huduma hizi angalau mara nne wanapo kuwa waja wazito. Pia wanafaa kupata huduma hizi punde tu wanapo jifungua mtoto. Iwapo kuna shida zozote zinazo shuhudiwa, mama anapaswa kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha ya mama na mtoto wake. Gharama ya huduma hizi ni ghali sana nchini Kenya. Kwa mwaka, inasemekana kuwa idadi hii ni asilimia 20 ya pesa zote za nchi kila mwaka zinazofikisha USD 1,380. Iwapo serikali ya Kenya inafanya juu chini ili wanawake wote nchini waweze kupata huduma hizi, bei bado inawalemea wananchi wengi. 

Gharama ya huduma za uja uzito kwa mama mwenye mimba nchini Kenya

Ni muhimu kwa kila mama mja mzito kupata huduma bora za ujauzito

Kuna juhudi kadhaa ambazo serikali imeweka kuhakikisha wamama wana pata huduma hizi

  • Kuondoa malipo ya huduma hizi. Iwapo serikali imepunguza malipo haya, bado wana wake waja wazito wanalipia huduma hii. Hii ni kwa sababu wanawake wengi wanatumia hospitali za kibinafsi na wala sio za serikali. Kuna sababu kadhaa zinazo wafanya waende hospitali hizi. Mara kwa mara, utapata wauguzi katika hospitali za serikali wamegoma. Hili ni tukio ambalo hutawai shuhudia katika hospitali za kibinafsi. Pia kuna laini ndefu sana katika hospitali za serikali. Mama anataka kuhudumiwa haraka ili arudi kazini ama kuwachunga watoto wake nyumbani. Unapata kuwa ana ngoja kwa muda mrefu ili apate huduma kwa hospitali za serikali. Katika hospitali za kibinafsi, huduma ni haraka na mama hangoji kwa muda mrefu. Ana uwezo wa kurudi kufanya shughuli zake.
  • Kliniki za kutembea – mobile clinics. Moja wapo ya juhudi za serikali ya nchi ya Kenya ya kuwasaidia wanawake waja wazito. Zinawasaidia wamama ila wakati mwingine unapata ziko katika kituo mbali na mama mja mzito. Kwa hivyo hawezi saidika kwani zina kaa zikienda mahala tofauti.
  • Serikali pia inataka kupitisha mswada wa huduma bure. Ambao utakuwa kwa hospitali zote nchini za serikali. Pia kutakuwa na chache za kibinafsi. Hizi zote ni juhudi za serikali kuhakikisha kuwa hawa wapotezi watoto ama wamama waja wazito kabla kujifungua ama wanapo jifungua.

Serikali inataka kuwafanya wamama wote waja wazito wenye uwezo mbali mbali wa maisha kupata huduma za uja uzito. Kupitia NHIF (National Hospital Insurance Fund) wamama waja wazito wana pata huduma hizi kwa bure. Ni muhimu kuwa elimisha wamama katika jamaa kuhusu njia wanayo weza kupata huduma hizi ili wasajiliwe. Baada ya hapo wanapo enda hospitalini kupata huduma za uja uzito, hawata hitajika kulipa chochote. 

Huduma za uja uzito nchini Kenya zimeshuhudia mabadiliko mengi . Kwa sasa wamama wengi waja wazito wanaweza faidika kutoka kwa huduma hizi. Gharama ya huduma za uja uzito ina stahili kuwa ya bei ya chini. Huduma hizi zinapokuwa huru kwa kila mama, itasaidia kuzuia vifo vya watoto wachanga na mama kabla ya kujifungua ama wanapo pata watoto.

Read Also: Pregnancy superstitions you probably didn’t know

Written by

Risper Nyakio