Je, ulifahamu kuwa sawa na binadamu, mbwa wa kike hupata kipindi cha hedhi?
Ilikuwa wikendi ya kufana. Huku watu wengi tukiliona jambo kwa mara ya kwanza. Tumesikia kuhusu watu kufanyia mbwa sherehe za sikukuu, kuweka mazishi, ila, kusherehekea kuwa na mimba? Mapya haya!

Gloria Kyallo, ndugu mdogo wa Betty Kyallo aliweka sherehe ya kufana ya mbwa wake Lulu mwenye mimba na anayetarajia kujifungua hivi karibuni.
Gloria na mchumba wake Ken waliwaalika marafiki wao wa karibu kwenye sherehe hii kusherehekea pamoja nao.

Katika picha alizoweka kwenye kurasa ya mtandao wake wa kijamii, Gloria aliandika. "Msichana wa lisaa. Heri za kusherehekea kila baraka. Napenda huyu msichana sana. Ana stahili haya na zaidi!!

Hongera kwa msichana wangu kwa kupata watoto wake wa kwanza," aliandika.
Katika mahojiano ya hapo awali, binti huyu alidhibitisha kuwa yeye ni mama wa mbwa na kuwa anamchukulia mbwa huyo kuwa mtoto wake. Hivi sasa ana mbwa watatu anao wapenda. Wanaishi na mamake katika nyumba yake huko Rongai.

Gloria Kyallo ndiye mtu mashuhuri wa kwanza nchini Kenya kuweka sherehe ya baby shower ya mbwa.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Kyallo Kulture: Betty Kyallo Na Dada Zake Wana Kipindi Kuhusu Maisha Yao