Hali Ya Watoto Wa Umri Chini Ya Miaka 5 Kukojoa Kitandani

Hali Ya Watoto Wa Umri Chini Ya Miaka 5 Kukojoa Kitandani

Kukojoa kitandani ni hali iliyo kawaida hasa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano na kwa kimombo maarufu kama enuresis. Ni ndoto la kila mzazi kuwa kadri mtoto wake anavyo zidi kukua, atawacha kukojoa kwenye kitanda chake. Mtoto anapo kua na kuendelea na hali hii, huenda jambo hili likamkwaza mzazi na kuanza kujiuliza maswali mengi. Ila, usiji kwaze mzazi, kuwa mtulivu na usitie shaka kwani haya yote ni kawaida. Ila, ni muhimu kwako na kila mzazi na wote wanao tarajia kuwa wazazi katika miaka ya hapo usoni kujua sababu zinazo wafanya watoto wa umri huu kuenda haja ndogo kitandani.

kukojoa kitandani

Sababu za Kukojoa Kitandani

Kulingana na utafiti uliofanyika, asilimia 16 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hushuhudia hali hii ya kuenda haja ndogo kwenye mahala pao pa kulala. Kadri wanavyo zidi kukua na kuongezeka miaka, hali hii hupungua wanapo fika miaka 15 hadi watoto wawili. Mtoto anaye shuhudia hali hii huenda akahisi kujitenga ama akatengwa na wanarika wake. Hasa ikiwa ako kwa shule ya bweni kwani hapo maisha yake yana julikana na wanafunzi wengine. Na huenda jambo hili likamkwaza. Makala haya yana azimio la kukujulisha sababu zinazo fanya mtoto wako kuwa na hali hii na jinsi ya kukabiliana na hali hii.

Kibofu cha mkojo kidogo

Kwa wakati mwingi, watoto wanao shuhudia hali hii huenda wakawa wana kibofu kidogo cha mkojo ambacho hakiwezi kusitira kiwango kikubwa cha mkojo. Na kumfanya mtoto kuenda haja ndogo anapokuwa amelala.

Kukosa maji tosha mwilini

Kukosa maji tosha mwilini kwa muda mrefu huenda kukaingilia uwezo wa kuthibiti wa kibofu cha mkojo kwani misuli yake inahusika katika kutoa kinya na mkojo.

watoto wa chini ya miaka 5

Kukwazwa kifikira

Ni jambo la kawaida kwa watoto kuwa na wasi wasi kabla ya matukio muhimu shuleni kama vile mitihani ama mambo mengine yanayo mfanya kuwa na fikira nyingi. Ila, kwa kesi hii, usitie shaka kwani baada ya tukio hilo kupita, ata rejelea hali yake ya hapo awali ya kulala vyema bila kuchafua kitanda chake.

Matatizo ya kiafya

Mara kwa mara, watoto wanao kabiliana na tatizo la kukojoa kitandani huenda wana matatizo ya kiafya. Je, matatizo hayo ni kama yepi? Mtoto aliye na maambukizo ya mfumo wa kukojoa (urinary tract infections), ugonjwa wa sukari na sleep apnea.

Historia ya familia

Iwapo wazazi wa mtoto huyu wana historia ya kukojoa kitandani, kuna uwezo mkubwa kuwa mtoto wako atakuwa anaenda haja ndogo kitandani.

Kulala sana

Watoto ambao hulala sana mara nyingi huwa na tatizo la kuenda haja ndogo kwenye kitanda.

Jinsia

Kukojoa usiku kwa mara nyingi huwa kawaida kwa wanaume kuliko kwa wanawake. Asilimia 2/3 ya watoto walio na hali ya kukojoa huwa wanaume wakati ambapo 1/3 huwa wanawake. Kadri miaka inavyozidi kupita asilimia hizi hubadilika na kuwa sawa wanapo fika miaka ya makamo maishani mwao. Kuunga mkono utafiti huu, wana sayansi wanasema kuwa sababu kuu ya jambo hili ni kuwa wanawake hukua kwa kasi zaidi kuliko wanaume.

Hali Ya Watoto Wa Umri Chini Ya Miaka 5 Kukojoa Kitandani

Jinsi ya kupambana na hali hii

Kengele za kukojoa kitandani

Kuna aina tofauti za kengele ambazo unaweza tumia kumwamsha mtoto wako wakati wa usiku ili aamke aende msalani. Unaweza ekelea karibu na meza kwenye chumba chake ama kwenye mguu wake. Wakati kengele ile inapolia, mtoto huamka na kwenda msalani ili kuepuka kukojoa mahala pake pa kulala.

Hata kama kuna madawa yanayo semekana kutibu hali hii, hakuna utafiti uano thibitisha jambo hili. Ila usitie shaka mzazi iwapo mtoto wako ana kumbana na hali hii. Kadri anavyozidi kuzeeka, hali hii itapungua kisha kuisha. Kuwa na utulivu. Iwapo mtoto wako atazidi kushuhudia hali hii ukubwani, hakikisha umepata ushauri wa daktari.

Vyanzo: Therapee, webmd

Written by

Risper Nyakio